Makundi ya Kipalestina: Msimamo wa uhasama wa Marekani kuhusu Palestina haubadiliki
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i64511-makundi_ya_kipalestina_msimamo_wa_uhasama_wa_marekani_kuhusu_palestina_haubadiliki
Makundi ya Kipalestina yametangaza kuwa kuingia madarakani Joe Biden hakutabadili msimamo wa kiuhasama wa Marekani kuhusu kadhia ya Palestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 09, 2020 00:58 UTC
  • Makundi ya Kipalestina: Msimamo wa uhasama wa Marekani kuhusu Palestina haubadiliki

Makundi ya Kipalestina yametangaza kuwa kuingia madarakani Joe Biden hakutabadili msimamo wa kiuhasama wa Marekani kuhusu kadhia ya Palestina.

Harakati ya Wananchi ya Ukombozi wa Palestina imetoa taarifa na kueleza kuwa, kile kitakachofanywa na Joe Biden Rais mteule wa Marekani ni kuendelea hatua zile za serikali zilizotangulia za chama cha Democratic za kuunga mkono Uzayuni. Makundi hayo ya Kipalestina aidha yametahadharisha kuhusu ahadi za uongo za serikali mpya ya Marekani za kurejea kwenye mazungumzo na Israel.  

Harakati ya Mujahiddin ya Palestina pia imesisitiza kuwa Trump na Biden wote wawili wanafanya kazi kwa maslahi ya utawala wa Kizayuni; na kuongeza kuwa serikali zote za Marekani zina sera zinazofanana. 

Mustafa al Barghuti Katibu Mkuu wa Harakati ya Ubunifu wa Kitaifa ya Palestina pia amemtaja Trump kuwa rais mbaya zaidi wa Marekani na kuongeza kuwa Trump amewatenda jinai kubwa dhidi ya wananchi wa Palestina. 

Mustafa al barghuthi, Katibu Mkuu wa Harakati ya Ubinifu wa Kiataifa ya Palstina 

Huko nyuma pia, Ismail Hania Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas, Khalid Mash'al Mkuu wa zamani wa harakati ya Hamas, Harakati ya Mujahiddin, kamati za muqawama za wananchi wa Palestina na viongozi wengine wa Palestina pia walitabiri kwamba, siasa za Biden mkabala na kadhia ya Palestina zitakuwa ni mwendelezo wa siasa zilezile za marais waliotangulia wa Marekani.