-
Jumanne Kuu na mustakbali wa uchaguzi wa Wademocrat nchini Marekani
Mar 05, 2020 08:36Siku muhimu zaidi katika kalenda ya uchaguzi wa mchujo wa urais wa Marekani ambayo imepewa jina la Jumanne Kuu katika kambi ya chama cha Democrats imemalizika kwa ushindi wa Joe Biden ambaye inaonekana ndiye atakayekabidhiwa bendera ya chama hiyo kwa ajili ya kupambana na Donald Trump katika uchaguzi wa mwishoni mwa mwaka huu wa 2020.
-
ICC yaamuru uchunguzi kuhusu jinai za kivita za Marekani nchini Afghanistan
Mar 05, 2020 08:24Majaji waandamizi katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) wameamuru uchunguzi uanze kuhusu jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu ambazo zinaripotiwa kufanywa na askari wa Marekani nchini Afghanistan.
-
Makundi ya muqawama Palestina yasisitiza kupambana na siasa haribifu za Marekani
Mar 04, 2020 08:24Makundi ya Muqawama huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu yamesisitiza juu ya kukabiliana na siasa haribifu za Marekani dhidi ya wananchi wa Palestina pamoja na njama za Kizayuni-Kimarekani kupitia mpango wa kibaguzi wa Muamala wa Karne.
-
CNN yakiri kwamba Iran inafanya juhudi kubwa kuvishinda virusi vya Corona
Mar 03, 2020 08:00Kanali ya televisheni ya CNN ya nchini Marekani imekiri kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, inafanya juhudi kubwa kuvishinda virusi hatari vya Corona.
-
Senegal na Saudia zaripoti kesi za kwanza za Corona, waliofariki Marekani wafika 6
Mar 03, 2020 04:00Saudi Arabia, Jordan na Tunisia ni nchi za hivi punde katika ulimwengu wa Kiarabu kuripoti kesi za kwanza za virusi vya Corona ambavyo vimeshaua watu zaidi ya elfu tatu kote duniani, hususan nchini China.
-
Pakistan: Hatuhitaji uingiliaji kati wa Marekani kutatua masuala yetu na Afghanistan
Mar 02, 2020 03:28Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan Shah Mahmood Qureshi amesema, hauhitajiki uingiliaji kati wa Marekani kwa ajili ya kutatuliwa masuala ya pande mbili kati ya nchi yake na Afghanistan.
-
Wamarekani wapandwa na wahka kwa kupotea "mask" za kupambana na Corona madukani
Mar 01, 2020 08:23Wakuu wa majimbo ya Marekani wameonya kuhusu wahka wa wananchi wa Marekani na kuongezeka mahitaji ya vifaa vya kupambana na virusi hatari vya corona wakisema kuwa, maduka makubwa ya nchi hiyo yamekumbwa na mgogoro wa upungufu wa vitendea kazi hivyo.
-
Marekani na al-Shabaab zalaumiana kuhusu mauaji ya raia Somalia
Mar 01, 2020 04:44Kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab limesema zaidi ya asilimia 80 ya mashambulizi ya anga yanayofanywa na Marekani nchini Somalia yanalenga raia wasio na hatia.
-
Washington yatangaza 'hali ya dharura' baada ya Corona kuua Marekani
Mar 01, 2020 04:33Gavana wa jimbo la Washington nchini Marekani ametangaza hali ya dharura ya kiafya baada ya mtu mmoja kuaga dunia kutokana na virusi vya Corona katika jimbo hilo, hii ikiwa ni kesi ya kwanza virusi hivyo kuua nchini Marekani.
-
Mamia waandamana katika miji ya US kulaani mauaji ya Waislamu India
Mar 01, 2020 04:26Mamia ya raia wa Marekani wenye asili ya India wamefanya maandamano katika miji mikubwa ya Marekani kulaani na kupinga ghasia zilizopelekea makumi ya watu kuuawa katika mji mkuu wa India, New Delhi.