-
Ulimwengu waunga mkono ripoti ya UN kuhusu mauaji ya kimbari ya Israel Ukanda wa Gaza
Mar 27, 2024 12:06Tathmini iliyofanywa na Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Masuala ya Palestina ambayo imezitaja jinai za utawala wa Kizayuni huko Ukanda wa Gaza kuwa ni mauaji ya kimbari imeungwa mkono pakubwa na nchi mbalimbali katika umoja huo.
-
Borrell: Israel inafanya mauaji ya halaiki dhidi ya watu wa Gaza
Mar 16, 2024 02:23Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya ambaye katika siku za hivi karibuni ameutuhumu utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa unatumia "njaa kama silaha" katika vita vya Gaza, ameonya kuwa utawala huo unawaua watu wa Gaza kwa umati.
-
Haniyeh awataka Wapalestina kuandamana kwenye Msikiti wa Al-Aqsa siku ya 1 ya Ramadhani
Feb 29, 2024 12:07Mkuu wa Ofisi ya Siasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amewataka Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na Israel kuandamana hadi Msikiti wa Al-Aqsa katika siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
-
Ukosoaji wa Iran kwa Baraza la Usalama la UN kwa kutochukua hatua kuhusiana na mauaji ya kimbari ya Wapalestina wa Ghazza
Feb 29, 2024 07:14Tangu ilipoanza duru mpya ya mauaji ya kimbari ya Wapalestina yanayofanywa na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghazza, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikitumia kila fursa inayopata kulaani jinai za utawala huo ghasibu na kutaka mashambulizi ya kinyama yanayofanywa dhidi ya Wapalestina yakomeshwe.
-
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran: Dhamiri zilizoamka zinapinga mauaji ya kimbari ya Wapalestina
Feb 27, 2024 12:42Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Iran amekitaja kilio cha rubani wa Marekani aliyejitoa mhanga kwa kujichoma moto mbele ya ubalozi wa Israel mjini Washington akipinga mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala huo dhidi ya watu wa Palestina huko Gaza kuwa ni sauti kubwa ya dhamiri zilizoamka nchini Marekani zinazopinga uungaji mkono wa serikali nchi hiyo kwa mauaji ya kimbari ya Wapalestina.
-
Rais wa Brazil: Kinachofanywa na Wazayuni huko Ghaza ni mauaji ya umati
Feb 24, 2024 06:19Rais Luiz Inácio Lula da Silva wa Brazil amesema kuwa, kinachofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel kwenye Ukanda wa Ghaza ni mauaji ya umati.
-
Mwakilishi wa Afrika Kusini ICJ: Israel imefanya mauaji ya kimbari Gaza
Feb 21, 2024 11:18Mwakilishi wa Afrika Kusini katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) ametangaza kuwa, uvamizi na mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza yanatisha zaidi kuliko mfumo wa ubaguzi wa rangi, apartheid.
-
Askari katili wa Israel wamuua baba na mama Wapalestina mbele ya watoto wao wadogo
Feb 16, 2024 03:25Katika muendelezo wa mauaji ya kimbari dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina katika Ukanda wa Ghazza, askari wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel wamewaua kwa kuwapiga risasi wazazi wa watoto kadhaa wa Kipalestina mbele ya macho yao.
-
Maoni: Wamarekani wanaamini Israel imefanya mauaji ya kimbari Gaza
Feb 09, 2024 02:33Nusu ya Wamarekani wanaamini kuwa, kumefanyika mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza huko Palestina.
-
Mahakama ya ICJ yaionya Israel na kuitaka iache kufanya mauaji ya kimbari Gaza
Jan 27, 2024 02:39Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) imeiamuru Israel iache vitendo vya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina, na kuchukua hatua za kuwasaidia raia.