Pars Today
Mawaziri watatu wa Misri yaani waziri wa biashara na viwanda, waziri wa mahakama na waziri wa fedha wamekumbwa na ugonjwa wa COVID-19.
Serikali ya Marekani imeidhinisha mauzo ya silaha zenye thamani ya dola milioni 200 kwa Misri licha ya serikali ya nchi hiyo kuendelea kuandamwa na shutuma za ukiukaji wa haki za binadamu.
Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika amekutana na kufanya mashauriano na viongozi wa Misri huko Cairo kuhusu bwawa la An Nahdhah.
Mahakama nchini Misri imewaweka viongozi 50 wa Harakati ya Ikhwanul Muslimin ya nchi hiyo katika orodha ya magaidi.
Kitengo cha upashaji habari cha Misri kimetangaza kuwa watuhumiwa wa masuala ya kisiasa wasiopungua 37 walinyongwa mwaka uliopita wa 2020 na watu wengine 75 waliaga dunia kwa uzembe wa kutopatiwa matibabu katika magereza ya Misri.
Wanajeshi wasiopungua wanane wa Misri wameuawa na kujeruhiwa baada ya gari lao kukanyaga bomu katika mkoa wa Sinai Kaskazini.
Katika mwendelezo wa siasa za White House zinazolenga kuuza silaha zaidi; Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani imetangaza kuwa imeafiki kutekelezwa mikataba ya kuziuzia silaha Misri, Kuwait na Saudi Arabia.
Gazeti la Washington Post limeripoti kuwa Saudi Arabia na Misri zimo kwenye orodha ya nchi hatari sana kwa waandishi habari katika mwaka huu wa 2020.
Serikali ya Misri imetangaza kuwa, karibuni hivi itafungua tena ubalozi wake katika nchi jirani ya Libya.
Katika kipindi cha mwezi mmoja wa hivi karibuni kumekuwa kukiripotiwa habari kuhusiana na kupatiwa ufumbuzi mgogoro baina ya Qatar na mataifa manne ya Kiarabu ya Saudi Arabia, Imarati, Misri na Bahrain.