Pars Today
Duru za habari za Misri zimearifu kuwa, serikali ya nchi hiyo inafanya jitihada ili kupokea awamu ya kwanza ya ndege za kivita kutoka Russia kabla ya kuingia White House Joe Biden Rais mteule wa Marekani.
Leo ni Ijumaa tarehe 3 Mfunguo Nane Jamadil Awwal mwaka 1442 Hijria mwafaka na tarehe 18 Desemba 2020 Miladia.
Safari ya hivi karibuni ya Rais Abdel Fattah el Sisi wa Misri nchini Ufaransa na mazungumzo aliyofanya na Rais Emmanuel Macron wa nchi hiyo vimeibua hasira na malalamiko ya waungaji mkono wa haki za binadamu.
Mashirika mengi ya haki za binadamu yamemtupia lawama chungu nzima Rais Abdel Fattah el Sisi wa Misri wakati huu wa ziara yake mjini Paris, Ufaransa.
Serikali ya Misri imewaachia huru wafanyakazi watatu wa shirika kubwa la kutetea haki za binadamu nchini humo kufuatia mashinikizo ya kimataifa.
Serikali ya Misri imeuonya utawala haramu wa Israel kwa hatua yake ya kutaka kujenga vitongoji vipya vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu ambazo zimepachikwa jina bandia la Israel.
Idadi kubwa ya wahadhiri wa vyuo vikuu na watetezi wa haki za binadamu kote ulimwenguni wamewataka viongozi wa serikali ya Misri iwaachie huru haraka iwezekanavyo wanachama watatu wa taasisi moja ya kutetea haki za binadamu ya nchini humo.
Majeshi ya Misri yametoa taarifa kuhusu mpango wa kufanyika luteka na mazoezi ya pamoja ya anga ya kijeshi kati ya nchi hiyo na Sudan katika anga ya Sudan.
Sheikh Mkuu wa al Azhar nchini Misri amekosoa matamshi ya chuki na hujuma ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa dhidi ya Uislamu na kutoa wito wa kutungwa sheria inayotambua chuki na uhasama dhidi ya Waislamu kuwa ni uhalifu.
Shirika la Maendeleo la Kiserikali la Nchi za Mashariki mwa Afrika (IGAD) limehimiza mazungumzo yafanyike na mwafaka ufikiwe ili kuleta suluhu kuhusu kadhia ya bwawa kubwa linalojengwa na Ethiopia kwenye Mto Nile linalojulikana kama Grand Renaissance Dam (GERD).