HRW yaitaka Saudi Arabia iwaachilie huru Wamisri 10 inaowashikilia
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i81486-hrw_yaitaka_saudi_arabia_iwaachilie_huru_wamisri_10_inaowashikilia
Shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Rights Watch limeutaka ukoo wa Aal Saud unaotawala kiimla nchini Saudi Arabia uwaachilie huru Wamisri 10 inaowashikilia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 17, 2022 07:24 UTC
  • HRW yaitaka Saudi Arabia iwaachilie huru Wamisri 10 inaowashikilia

Shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Rights Watch limeutaka ukoo wa Aal Saud unaotawala kiimla nchini Saudi Arabia uwaachilie huru Wamisri 10 inaowashikilia.

Mahakama maalumu ya Riyadh ya kusikiliza kesi za watu wanaotuhumiwa kufanya ugaidi, imeanza kusikiliza kesi ya raia 10 wa Misri wanaotuhumiwa kufanya sherehe za ushindi wa Oktoba 6 (vita vya tarehe 6 Oktoba 1973) na tuhuma nyinginezo za haki binadamu, haki za raia na uhuru wa kujieleza. Wamisri hao ni wa kabla la Nubi ambao eneo lao liko kaskazini mwa Sudan na kusini mwa Misri.

Human Rights Watch ni shirika la kimataifa lisilo la kiserikali na makao yake makuu yako mjini New York Marekani. Leo Alkhamisi, shirika hilo limeutaka ukoo wa Aal Saud huko Saudi Arabia kuwaachilia huru raia hao 10 wa Misri wa kabila la Nubi ambao wamefungwa jela nchini humo kidhulma na kinyume cha sheria.

 

Mwito huo umetolewa huku kila upande duniani ukiendelea kulaani jinai ya siku ya Jumamosi ya kuuliwa kwa umati tena siku moja watu 81 nchini Saudi Arabia kwa maidai kufanya makosa yasiyosahemeka.

Rais wa zamani wa Tunisia, Moncef Marzouki naye amelaani kuuliwa kwa umati watu hao 81 katika siku moja na kusema kuwa utawala wa ukoo wa Aal Saud umetumia vibaya fursa ya kushughulishwa dunia na vita vya Ukraine, kufanya jinai hiyo, lakini ijiandae kwa matokeo yake mabaya.

Ni vyema tukumbushe hapa kwamba, 41 kati ya watu hao 81 waliotekelezewa adhabu ya kifo kwa siku moja huko Saudia, walikuwa ni vijana wa Kishia wa eneo la Qatif la nchi hiyo..