Pars Today
Jeshi la Misri limetangaza habari ya kuangamizwa magaidi 13 katika muendelezo wa operesheni za wanajeshi wa nchi hiyo katika Rasi ya Sinai.
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Misri ametaka kufuatiliwa kwa kina na kwa karibu shughuli za vyombo vya habari na kuchukuliwa hatua za kisheria dhidi ya chombo chochote cha habari ambacho kinavuruga usalama na kuhatarisha maslahi ya taifa.
Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch (HRW) limeikosoa serikali ya Misri kwa hatua yake ya kuwatia mbaroni kiholela wanasiasa wa upinzani nchini humo.
Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa serikali ya Misri imetoa amri ya kuzuiliwa mali zote za mkuu wa chama cha Misri Imara ambaye alitiwa mbaroni hivi karibuni baada ya kumkosoa Rais Abdel Fattah el Sisi wa nchi hiyo.
Kamepeni za uchaguzi wa Rais Misri zilianza Jumamosi huku Rais Abdel Fattah el-Sisi akitazamiwa kupata ushindi kwa urahisi baada ya wapinzani wake asili kukamatwa, kufungwa jela au kutishwa na hivyo kujiondoa katika mchuano huo.
Leo ni Jumamosi tarehe 7 Mfunguo Tisa Jamadi Thani 1439 Hijria mwafaka na tarehe 24 Februari 2018 Miladia.
Serikali ya Misri imemuweka kiongozi wa chama cha upinzani cha "Misri Imara" na wanachama wengine 15 wa chama hicho katika orodha ya magaidi.
Misri imekubali ombi la Ethiopia la kuakhirisha mkutano wa pande mbili wa kujadili suala tata la bwawa la al-Nahdha linalojengwa na Uhabeshi, baada ya Adiss Ababa kutangaza sheria ya hali ya hatari.
Jeshi la Misri limetangaza kuwaaangamiza magaidi saba wakufurishaji katika oparesheni maalumu ya kijeshi inayoendelea katika eneo la Sinai nchini humo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri ameonya kuwa magaidi wa Daesh (ISIS) waliosafishwa huko Syria na Iraq wanafanya kila wawezalo kuzivamia nchi za kaskazini mwa Afrika hususan Libya.