Kampeni za uchaguzi wa rais Misri zaanza
(last modified Sun, 25 Feb 2018 07:28:51 GMT )
Feb 25, 2018 07:28 UTC
  • Kampeni za uchaguzi wa rais Misri zaanza

Kamepeni za uchaguzi wa Rais Misri zilianza Jumamosi huku Rais Abdel Fattah el-Sisi akitazamiwa kupata ushindi kwa urahisi baada ya wapinzani wake asili kukamatwa, kufungwa jela au kutishwa na hivyo kujiondoa katika mchuano huo.

Sisi amekuwa madakrani tangu anyakue madaraka mwaka 2013 kupitia mapinduzi ya kijeshi ambapo rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini humo, Mohammad Morsi, alitimuliwa madarakani baada ya kutawala kwa mwaka mmoja tu.

Wagombea wengine  katika uchaguzi wa rais Misri ni Moussa Moustafa Moussa, wa chama kinachounga mkono serikali cha Ghad (Kesho). Moussa aliwasilisha makaratasi yake ya kugombea urais dakika chache kabla ya muhula kumalizika na kama hangefanya hivyo Sisi angekuwa ndiye mgombea pekee.

Kampeni za uchaguzi zitaendelea hadi Machi 13 na uchaguzi umepangwa kufanyika Machi 26-28 na iwapo mshindi hatakapitakana katika duru ya kwanza duru ya pili itafanyika Aprili 24-26.

Abdul Futuh

Watu milioni sitini wametimiza masharti ya kupiga kura katika uchaguzi huo.

Katika kuwakandamiza wapizani serikali ya Misri hivi karibuni ilimuweka kiongozi wa chama cha upinzani cha "Misri Imara" Abul Futuh na wanachama wengine 15 wa chama hicho katika orodha ya magaidi. Futuh alikuwa na nia ya kugombea uchaguzi.

Miongoni mwa  wanasiasa wa upinzani waliotiwa nguvuni nchini Misri ni Sami Hafez Anan, mkuu wa zamani wa jeshi la nchi hiyo aliyekuwa ametangaza kuwa atachuana na Sisi katika uchaguzi ujao.

Tags