-
Morocco, Saudia na Imarati zaingia katika ugomvi mkubwa, Rabat yawaita nyumbani mabalozi wake
Feb 09, 2019 21:46Morocco, Saudia na Imarati zimeingia katika ugomvi mkubwa na kuifanya serikali ya Rabat iwaite nyumbani mabalozi wake kutoka Abu Dhabi na Riyadh.
-
Morocco yajitoa kwenye muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudia dhidi ya Yemen
Feb 08, 2019 03:26Maafisa wa serikali ya Morocco wametangaza kuwa nchi hiyo imesita kushiriki kijeshi katika kile kinachoitwa muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia katika vita dhidi ya Yemen na imechukua hatua ya kumwita balozi wake wa mjini Riyadh.
-
UN yapinga madai ya Morocco kuhusu Polisario
Jan 14, 2019 03:46Umoja wa Mataifa umepinga madai ya Morocco ya kwamba Harakati ya Polisario ya ukombozi wa Sahara Magharibi imevunja makubaliano ya kusimamisha vita na kusisitiza kuwa, hakuna ushahidi wowote unaoonesha kuwa Polisario imevunja makubaliano hayo.
-
Morocco yawatia nguvuni walioua watalii wa Norway na Denmark
Dec 22, 2018 11:48Serikali ya Morocco imewatia nguvuni watu 9 wanaotuhumiwa kuwa ndio waliwaua wataali wawili wa kike kutoka nchi za Denmark na Norway.
-
Jitihada za kuboresha hali za wahajiri duniani
Dec 10, 2018 23:05Mkutano wa kimataifa wa uhajiri ulianza jana Jumatatu ya tarehe 10 Desemba nchini Morocco katika hali ambayo, mazingira na hali isiyoridhisha ya kisiasa, kijamii na kiuchumi, pamoja na kukosekana usalama katika nchi mbalimbali duniani hususan za mabara ya Afrika na Amerika ya Latini na maeneo mengine kadhaa ya bara la Asia vimesababisha kuongezeka wimbi la wahajiri duniani.
-
Nchi zaidi ya 150 zapasisha Mkataba wa Kimataifa wa Wahajiri licha ya upinzani wa Marekani
Dec 10, 2018 11:46Zaidi ya nchi 150 duniani zimeunga mkono rasmi Mkataba wa Kimataifa wa Wahajiri katika mkutano unaofanyika nchini Morocco licha ya upinzani mkubwa wa Marekani.
-
Kutofanikiwa mazungumzo ya Morocco na Harakati ya Polisario mjini Geneva; sababu na mustakabali
Dec 09, 2018 04:22Kikao cha Morocco na Harakati ya Polisario kuhusu hitilafu za eneo la Sahara Magharibi kimefanyika mjini Geneva Uswisi chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa na kilimalizika bila natija.
-
Miili ya wahajiri 15 yapatikana ndani ya boti katika bahari ya Mediterania
Nov 25, 2018 04:45Maiti za wahajiri 15 wa Kiafrika zimepatikana na jeshi la majini la Morocco, zikiwa ndani ya boti iliyokuwa ikielea katika bahari ya Mediterania.
-
Algeria na Mauritania zakutana kuzungumzia Sahara Magharibi
Oct 22, 2018 23:32Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Algeria na Mauritania wameitisha kikao cha pamoja cha kujadili hatima ya Sahara Magharibi inayopigania uhuru wake kutoka kwa Morocco.
-
Morocco yazuia maelfu ya wahajiri haramu kutumia ardhi ya nchi hiyo
Sep 07, 2018 20:53Viongozi wa Morocco wametangaza kuwa, tangu mwanzoni mwa mwaka huu hadi hivi sasa, serikali ya nchi hiyo imefanikiwa kuzuia wahajiri haramu 54 elfu kutumia ardhi ya nchi hiyo kuelekea barani Ulaya.