Morocco yawatia nguvuni walioua watalii wa Norway na Denmark
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i50346-morocco_yawatia_nguvuni_walioua_watalii_wa_norway_na_denmark
Serikali ya Morocco imewatia nguvuni watu 9 wanaotuhumiwa kuwa ndio waliwaua wataali wawili wa kike kutoka nchi za Denmark na Norway.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 22, 2018 11:48 UTC
  • Morocco yawatia nguvuni walioua watalii wa Norway na Denmark

Serikali ya Morocco imewatia nguvuni watu 9 wanaotuhumiwa kuwa ndio waliwaua wataali wawili wa kike kutoka nchi za Denmark na Norway.

Polisi ya mji wa Rabat imetangaza kuwa, imewakamata washukiwa hao ambao waliwaua kwa kuwadunga kisu Louisa Vesterager Jespersen kutoka Denmark na Maren Ueland wa Norway.

Maiti za watalii hao zilikutwa katika maeneo ya milimani ya kusini magharibi mwa nchi hiyo zikiwa na alama za kudungwa kisu.

Watalii hao waliuawa wakiwa njiani kuelekea kwenye mlima mrefu zaidi wa kaskazini mwa Afrika wa Toubkal.

Louisa Vesterager Jespersen na Maren Ueland 

Ofisi ya mwendesha mashtaka wa wa serikali ya Morocco imesema kuwa baadhi ya washukiwa hao ni wanachama wa kundi la kigaidi la Daesh.

Mapema leo mamia ya watu walifanya maandamano mbele ya balozi za Denmark na Norway mjini Rabat wakitangaza mshikamano wao na wahanga hao na familia zao na kupinga ugaidi wa aina zote nchini Morocco.