Pars Today
Waziri Mkuu wa Italia Paolo Gentilon amesema atapendekeza katika bunge la nchi hiyo kuwa baadhi ya wanajeshi wa Italia walio Iraq wapelekwe Niger kupambana na biashara haramu ya usafirishaji binadamu na ugaidi.
Rais wa Ufaransa amewasili Niger kwa lengo la kukutana na wanajeshi wa nchi hiyo na kuchunguza hali ya mambo katika nchi za magharibi mwa Afrika.
Umoja wa Mataifa umeanza zoezi la kuwahamisha wakimbizi wa nchi za Afrika walioko Libya na kuwapeleka nchini Niger.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Rais wa Niger wamesisitiza suala la kukuza uhusiano wa kisiasa kati ya pande mbili na kupambana na ugaidi.
Waziri wa mambo ya Ndani wa Niger ametangaza habari ya kuuawa wanajeshi 12 wa nchi hiyo katika shambulio jipya lililotokea kwenye mpaka wa nchi hiyo na Mali, kaskazini magharibi mwa Niger.
Kuuliwa wanajeshi wanne wa Marekani nchini Niger kumezidi kutoa mguso juu ya suala la kuhalalishwa kuongezwa idadi ya wanajeshi wa Marekani barani humo.
Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon, imethibitisha kuuawa Komando wa nne wa jeshi la nchi hiyo katika hujuma ya kuvizia nchini Niger ambapo awali ilikuwa imetangazwa ni makomnando watatu waliouawa.
Makomando watatu wa kikosi maalumu cha jeshi la Marekani wameuawa katika shambulizi la kuvizia nchini Niger wakiwa katika oparesheni ya kutoa mafunzo kwa jeshi la nchi hiyo.
Kutokana na kuendelea mashambulio ya kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram katika eneo la magharibi mwa Afrika viongozi wa serikali ya Niger wametoa onyo kwa wafanyabiashara wanaoshirikiana kibiashara au kwa namna yoyote ile na kundi hilo.
Viongozi wa Niger wamewaonya vikali wafanyabiashara ambao wanafanya biashara kwa siri na kundi la kigaidi la Boko Haram.