-
Waislamu Nigeria wakanusha madai ya polisi kumhusu Zakzaky
Nov 18, 2019 08:18Wafuasi wa Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria wamekanusha vikali madai ya Idara ya Kiitelejensia ya Nigeria kuwa polisi ya nchi hiyo inamzuilia mwanaharakati huyo wa Kiislamu kutokana na ombi na uamuzi wake mwenyewe.
-
Wakimbizi laki moja wakwama kambini kwa mafuriko Nigeria
Nov 13, 2019 23:12Wakimbizi wa Ndani (IDPs) zaidi ya laki moja wameshindwa kutoka makambini kutokana na mafuriko makubwa yaliyolikumba jimbo la Borno la kaskazini mashariki mwa Nigeria.
-
Watu zaidi ya 60 waaga dunia kwa ugonjwa wa kutatanisha uliozuka kaskazini ya Nigeria
Oct 30, 2019 23:03Ugonjwa wa kutatanisha uliozuka katika jimbo la Katsina kaskazini mwa Nigeria umeua zaidi ya watu 60 katika jimbo hilo.
-
Ufichaji mambo wa serikali ya Nigeria kuhusiana na hali ya Sheikh Zakzaky
Oct 27, 2019 23:08Familia ya Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria imetangaza kuwa, serikali ya nchi hiyo imekuwa ikificha na kukataa kutoa taarifa kuhusiana na hali ya kiafya ya kiongozi huyo pamoja na mkewe.
-
Polisi ya Nigeria yakomboa 'wanafunzi' wengine 150 Kaduna
Oct 20, 2019 04:12Polisi nchini Nigeria kwa mara nyingine tena imefanikiwa kuwaokoa watoto na vijana mabarobaro wapatao 150 kutoka katika kituo kimoja ambako walikuwa wakifanyiwa mateso kaskazini mwa nchi.
-
Polisi Nigeria yatumia risasi na mabomu kuvunja Arubaini ya Imam Hussein AS
Oct 19, 2019 09:50Polisi nchini Nigeria imetumia risasi hai na mabomu ya gesi ya kutoa machozi kuvunja matembezi ya amani ya waumini wa Kiislamu waliokuwa wakishiriki maombolezo ya Arubaini ya Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) katika mji mkuu Abuja.
-
Nigeria: Hakuna fedha za kutosha kwa ajili ya kupambana na Boko Haram
Oct 16, 2019 22:09Mwenyekiti wa Kamisheni ya Ulinzi ya Bunge la Nigeria ametangaza kuwa, serikali ya nchi hiyo haina fedha za kutosha kwa ajili ya kugharamia mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la Boko Haram
-
Jeshi la Nigeria lasafisha maeneo ya kaskazini na kuangamiza waasi
Oct 08, 2019 03:07Jeshi la Nigeria limetangaza kuwa limeangamiza waasi wasiopungua 10 katika operesheni iliyofanyika kwenye misitu ya karibu na maeneo ya Birnin Gwari na Janko Hill huko Kaduna yanayosumbuliwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya magenge yanayobeba silaha.
-
Magaidi wa Boko Haram waua watu 27 Nigeria
Oct 06, 2019 08:30Watu 27 wamepoteza maisha kaskazini mashariki mwa Nigeria kufuatia shambulizi la kigaidi ambalo limetekelezwa na kundi la Boko Haram linalofungamna na kundi la kigaidi la ISIS (Daesh).
-
Walioteka nyara wanafunzi wa kike Nigeria wataka kikomboleo
Oct 05, 2019 23:20Watu wenye silaha waliowateka nyara wanafunzi sita wa kike wa chuo kimoja pamoja na wafanyakazi wawili wa chuo hicho huko Kaduna Nigeria, wametaka walipwe fedha za kuwakombolea mateka hao.