Jeshi la Nigeria lasafisha maeneo ya kaskazini na kuangamiza waasi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i56485-jeshi_la_nigeria_lasafisha_maeneo_ya_kaskazini_na_kuangamiza_waasi
Jeshi la Nigeria limetangaza kuwa limeangamiza waasi wasiopungua 10 katika operesheni iliyofanyika kwenye misitu ya karibu na maeneo ya Birnin Gwari na Janko Hill huko Kaduna yanayosumbuliwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya magenge yanayobeba silaha.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 08, 2019 03:07 UTC
  • Jeshi la Nigeria lasafisha maeneo ya kaskazini na kuangamiza waasi

Jeshi la Nigeria limetangaza kuwa limeangamiza waasi wasiopungua 10 katika operesheni iliyofanyika kwenye misitu ya karibu na maeneo ya Birnin Gwari na Janko Hill huko Kaduna yanayosumbuliwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya magenge yanayobeba silaha.

Taarifa iliyotolewa na jeshi la Nigeria imesema kuwa, wanachama 10 wa kundi moja la wabeba silaha wameuawa katika operesheni hiyo iliyofanyika katika jimbo la Kaduna kaskazini magharibi mwa Nigeria. 

Afisa mawasiliano wa kikosi cha Jeshi la Anga la Nigeria, Ibikunle Daramola amesema operesheni hiyo imefanyika kwa ushirikiano wa vikosi vya majeshi ya anga na nchi kavu na kwamba idadi kubwa ya wanachama wa genge hilo wamejeruhiwa. 

Mashambulizi yanayofanywa na magenge ya waasi na mapigano ya kikabila na kikaumu katika maeneo mbalimbali ya Nigeria yanatoa changamoto kubwa kwa serikali ya Rais Muhammadu Buhari.

Wapiganaji wa kundi la kigaidi la Boko Haram

Nigeria pia inasumbuliwa na mashambulizi ya kundi la kigaidi la Boko Haram ambalo hadi sasa limeua watu zaidi ya elfu 35 tangu lilipoanzisha hujuma nchini Nigeria na katika nchi jirani. Mamilioni ya watu pia wamelazimika kuwa wakimbizi kutokana na mashambulizi ya kundi hilo.