-
Matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa Pakistan
Feb 13, 2024 07:18Tume ya Uchaguzi ya Pakistani imetangaza matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa bunge nchini humo, na wagombea huru wenye mfungamano na chama cha Tehreek-e-Insaf cha Imran Khan wamenyakua viti 101.
-
Mamilioni ya Wapakistan wapiga kura kuchagua serikali mpya, matukio kadhaa ya mauaji yaripotiwa
Feb 08, 2024 11:33Wapakistani wapatao milioni 128 waliotimiza masharti leo wameelekea kwenye vituo vya kupigia kura katika uchaguzi mkuu muhimu wa kuchagua serikali mpya itakayoongoza nchi hiyo kwa miaka mitano ijayo, huku usalama ukiimarishwa kwa kuchukuliwa hatua kadhaa ikiwemo kusitishwa huduma za simu za mkononi na mtandao wa intaneti licha ya kuripotiwa matukio kadhaa ya mauaji.
-
Maelfu ya watoto wanaugua nimonia nchini Pakistan
Feb 05, 2024 03:14Maafisa husika wa Afya wameripoti kutoka Pakistan kuwa watoto zaidi ya 19,000 katika jimbo la Punjab kaskazini mashariki mwa nchi hiyo wamegunduliwa kuugua maradhi ya homa ya mapafu yaani nimonia (Pneumonia) baada ya kufanyiwa vipimo katika kipindi cha mwezi mmoja wa karibuni.
-
Mipaka ya Iran na Pakistan kubadilishwa kuwa ya kiuchumi na kiurafiki
Feb 01, 2024 02:59Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, juhudi zinafanyika kuhakikisha kwamba, mipaka ya nchi yake na Pakistan inabadilika na kuwa ya kiuchumi, amani na urafiki.
-
Imran Khan na msaidizi wake wahukumiwa kifungo cha miaka 10 jela kwa kuvujisha siri za Serikali ya Pakistan
Jan 31, 2024 02:40Mahakama ya Pakistan imemhukumu waziri mkuu wa zamani Imran Khan na msaidizi wake wa karibu, waziri wa zamani wa mambo ya mje Shah Mahmood Qureshi, kifungo cha miaka 10 jela katika kesi inayohusiana na uvujaji wa siri za serikali.
-
Amir Abdollahian: Iran na Pakistan zimekubaliana kupanua ushirikiano wa kupambana na ugaidi
Jan 30, 2024 11:09Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa Tehran na Islamabad zimekubaliana kupanua ushirikiano kwa ajili ya kupambana na ugaidi.
-
Tehran: Iran na Pakistan hazitaruhusu maadui waharibu uhusiano wao wa kindugu
Jan 28, 2024 07:54Kufuatia shambulio lililowalenga raia wa Pakistan ndani ya Iran, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema Tehran na Islamabad hazitavumilia chokochoko za kuharibu uhusiano wa nchi hizo mbili.
-
Mapigano yazuka kati ya majeshi ya Pakistan na Afghanistan kwenye mpaka wa nchi mbili
Jan 21, 2024 11:25Mapigano yamezuka kati ya vikosi vya mpakani vya jeshi la Pakistan na vya utawala wa Taliban ya Afghanistan katika eneo la mpaka wa nchi hizo mbili.
-
Pakistan yatangaza kurejesha uhusiano kamili na Iran baada ya mivutano iliyojitokeza
Jan 20, 2024 06:53Pakistan imetangaza kurejesha kikamilifu uhusiano wa kidiplomasia na Iran baada ya kujitokeza mivutano mikali ya mpakani ambayo haijawahi kushuhudiwa kati ya nchi mbili juu ya operesheni za kupambana na ugaidi.
-
Azma thabiti ya Iran na Pakistan ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kupambana na ugaidi
Jan 20, 2024 03:00Baada ya kushadidi mivutano ya mpakani kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Pakistan katika kipindi cha siku mbili zilizopita, viongozi wa Tehran na Islamabad wamesisitiza kuendeleza uhusiano wa kirafiki kati ya nchi mbili, kuheshimiwa umoja wa ardhi za mataifa hayo mawili na kuwepo uratibu na mashauriano ya karibu zaidi katika kupambana na magenge ya kigaidi.