-
Tovuti ya Uingereza: Utawala wa Marekani ni kipofu kiasi kwamba unamhami mtu kama Netanyahu
Jul 29, 2024 22:59"Kuporomoka kwa dola kunakuwa jambo lisiloepukika mara tu watawala wake wanapopoteza kabisa hisia za jinsi walivyokuwa wapuuzi na wa kutisha", hivi ndivyo ilivyoandika tovuti ya Uingereza ya Middle East Eye ikizungumzia fedheha kubwa ya Congress ya Marekani ya kumkaribisha na kumpigia makofi nduli na Adolf Hitler wa zama hizi, Benjamin Netanyahu, anayeendelea kufanya mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza huko Palestina.
-
Ripoti ya mashirika ya UN: Ghaza ina hali mbaya zaidi ya uhaba wa chakula duniani
Jul 27, 2024 08:05Ripoti mpya ya pamoja iliyotolewa na mashirika matano ya Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa Ukanda Ghaza uliowekewa mzingiro na kuzuiliwa na jeshi la Kizayuni kuingiziwa misaada ya chakula, ndilo eneo linalokabiliwa na hali mbaya zaidi ya ukosefu wa chakula duniani.
-
HAMAS: Kauli ya Marekani ni uongo mtupu, Wapalestina Ghaza wanauawa kwa silaha zake
Jul 26, 2024 09:29Mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema: "Madai ya Washington kwamba inatiwa wasiwasi na hali ya kibinadamu na inasikitishwa na machungu na mateso wanayopata watu wa Ghaza ni uongo wa Kimarekani".
-
Amnesty International: Marekani mshirika wa Israel katika mauaji ya kimbari Palestina
Jul 25, 2024 03:41Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International imeonya Marekani kuhusu kuupa silaha utawala wa Kizayuni katika vita vya Gaza na kutangaza kuwa, Washington ni mshirika wa utawala huo katika mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina.
-
Kufanyika kura ya maoni Palestina; mkakati na suluhisho la Iran
Jul 23, 2024 10:29Nasser Kanani, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema kuwa, "suluhisho bora zaidi la kuhitimisha hali haramu ya sasa katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu ni kufanyika kura ya maoni jumuishi kwa kushirikisha wakaazi wote na raia asili wa ardhi hiyo."
-
Ripota wa Umoja wa Mataifa akosoa vitendo vya kibaguzi vya utawala wa Israel
Jul 22, 2024 22:55Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa Kuhusu Haki za Binadamu huko Palestina amekosoa mienendo ya kikatili ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina.
-
Mandela: Houthi wazidishe mashambulizi ili kuikomboa Palestina
Jul 22, 2024 07:28Mjukuu wa Nelson Mandela, shujaa na kiongozi wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini ametoa mwito kwa Harakati ya Ansarullah na vikosi vya wanajeshi wa Yemen kushadidisha operesheni zao dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel unaoendelea kuua watoto na wanawake wasio na hatia katika Ukanda wa Gaza.
-
Jumatatu, Julai 22, 2024
Jul 21, 2024 22:59Leo ni Jumatatu tarehe 16 Mfunguo Nne Muharram 1446 Hijria sawa na Julai 22, 2024 Milaadia.
-
Iran yapongeza hukumu ya ICJ, yataka kura ya maoni kuamua mustakbali wa Palestina
Jul 20, 2024 23:04Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, njia bora zaidi ya kulipatia ufumbuzi suala la Palestina na kukomeshwa jinai za utawala haramu wa Israel, ni kufanyika kura ya maoni itakayowashirikisha Wapalestina wa ardhi zote za taifa hilo ili waamue mustakbali wao.
-
Riyadh yaipongeza ICJ kuvitaja vitongoji vya Wazayuni kuwa haramu
Jul 20, 2024 04:24Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia imekaribisha uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) wa kuvitaja vitongoji ya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) kuwa ni kinyume cha sheria.