Riyadh yaipongeza ICJ kuvitaja vitongoji vya Wazayuni kuwa haramu
(last modified Sat, 20 Jul 2024 07:54:08 GMT )
Jul 20, 2024 07:54 UTC
  • Riyadh yaipongeza ICJ kuvitaja vitongoji vya Wazayuni kuwa haramu

Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia imekaribisha uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) wa kuvitaja vitongoji ya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) kuwa ni kinyume cha sheria.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudia imesema katika taarifa yake kwamba, nchi hiyo imekaribisha uamuzi wa ushauri wa Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ) na kusisitiza kwamba; uwepo wa utawala katili wa Israel katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu  na Israel tangu miaka 57 iliyopita ni haramu na usio kubalika kabisa.

Riyadh yapongeza uamuzi wa ICJ kuyaita makazi ya Israel kuwa haramu 

Mahakama ya Juu ya Umoja wa Mataifa ilitangaza uamuzi huo siku ya Ijumaa kuhusu vitongoji 230 zaidi vya walowezi ambavyo vimejengwa katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, ikiwemo Quds Mashariki, tangu utawala huo ulipokalia kwa mabavu ardhi ya Palestina mwaka 1967, na kuzingira kila eneo la watu hao wasio na ulinzi wala hatia huko Ukanda wa Gaza.

Mahakama ilibainisha kuwa, ujenzi na uwepo kwa majengo ya walowezi wa Kizayuni katika eneo hilo unaweza kuhesabiwa kuwa ubaguzi na mfumo wa ubaguzi wa rangi (apartheid).