Pars Today
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Qatar ameionya Saudi Arabia kuhusiana na kuchukua hatua yoyote ya kijeshi dhidi ya nchi yake.
Vyanzo vilivyo karibu na Haidar al-Abadi Waziri Mkuu wa Iraq vimesema kuwa Saudi Arabia inaishiinikiza nchi hiyo ili ijiunge na nchi zinazoiwekea vikwazo Qatar
Kuongezeka mivutano katika uhusuano wa nchi nne za Kiarabu na Qatar kumezisababishia madhara makubwa ya kiuchumi nchi za Saudia na Imarati.
Misri imeifungia Qatar njia zote za majini zinazotumiwa na meli za Qatar isipokuwa mfereji wa Suez.
Mwakilishi mmoja wa Bunge la Misri amefichua baadhi ya hatua zinazotarajiwa kuchukuliwa katika siku zijazo na Saudi Arabia, Imarati, Bahrain na Misri dhidi ya Qatar.
Serikali ya Marekani imesema ina wasiwasi wa uwezekano wa kuongezeka hali ya mvutano kati ya Qatar na Saudi Arabia.
Saudi Arabia na waitifaki wake zimetoa taarifa ya pamoja na kudai kuwa hatua ya Qatar ya kukataa masharti ya nchi nne za Kiarabu zilizoiwekea vikwazo vya kila namna nchi hiyo inaonesha nia ya Doha ya kuhatarisha usalama na utulivu wa eneo hili.
Katika hali ambayo Qatar inakabiliwa na mgogoro wa kidiplomasia na mzingiro wa nchi nne za Kiarabu, nchi hiyo sasa imeamua kuongeza uzalishaji wake wa gesi asilia hadi asilimia 30 katika kipindi cha miaka kadhaa ijayo.
Kwa mara nyingine Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Marekani na Misri wameituhumu Qatar kwamba, inaunga mkono ugaidi, kuingilia masuala ya ndani ya nchi majirani na kufanya mahusiano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Waziri wa Ulinzi wa Qatar amesema jeshi la nchi hiyo liko tayari kuilinda nchi hiyo endapo itakabiliwa na chokochoko tarajiwa za maadui.