Qatar: Tunaishitaki Saudia kwa kutishia kushambulia ndege zetu za abiria
(last modified Mon, 21 Aug 2017 08:23:20 GMT )
Aug 21, 2017 08:23 UTC
  • Qatar: Tunaishitaki Saudia kwa kutishia kushambulia ndege zetu za abiria

Serikali ya Qatar imetangaza kuwa imekusudia kuishitaki Saudi Arabia katika Umoja wa Mataifa kutokana na nchi hiyo kutishia kuzishambulia ndege zake za abiria.

Taarifa iliyotolewa Jumapili ya jana na Doha sambamba na kukosoa ripoti ya televisheni moja ya Saudia kuhusu vitisho hivyo imesema kuwa, Qatar inaitambua ripoti hiyo kuwa ni njia ya kuzusha hofu na wasiwasi kwa wasafiri wanaotumia ndege zenye bendera ya taifa hilo. Hivi karibuni televisheni ya taifa ya Saudia ilitangaza kuwa, nchi washirika zilizoiwekea vikwazo Qatar zinayo haki ya kuzishambulia ndege za abiria za nchi hiyo iwapo ndege hizo zitakaribia anga yao.

Bendera za nchi zilizoiwekea vikwazo Qatar

Kufuatia ripoti hiyo, serikali ya Doha imeitaja taarifa hiyo kuwa ni ukiukaji wa wazi wa mikataba na makubaliano ya kimataifa.

Wakati huo huo na katika kuendelea kutokota kwa mgogogro wa mataifa ya Kiarabu ya eneo la Ghuba ya Uajemi, Dhahi Khalfan Tamim, Naibu Mkuu wa Polisi ya Dubai ametaka kusimamishwa uanachama wa Qatar katika Baraza la Ushirikiano wa Ghuba ya Uajemi na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League). Khalfan pia amedai kuwa balozi za Qatar katika pembe mbalimbali za dunia zimekuwa zikitumika kuyavutia makundi ya kigaidi na kushirikiana nayo.

Dhahi Khalfan Tamim, Naibu Mkuu wa Polisi mjini Dubai

Saudia, Imarat, Bahrain na Qatar zilitangaza kukata mahusiano yao na serikali ya Qatar hapo tarehe tano mwezi Juni mwaka huu zikiituhumu nchi hiyo kuwa inaunga mkono ugaidi. Mbali na hayo ni kwamba nchi hizo ziliiwekea mzingiro wa kila upande Qatar kuanzia baharini, angani na nchi kavu.

Tags