-
Hamas yasema kesho ni 'Ijumaa ya Ghadhabu' ya kuihami Quds
Dec 07, 2017 11:20Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas imeutaja uamuzi wa Rais wa Marekani, Donald Trump wa kuitangaza Baytul Muqaddas kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel kama tangazo la vita huku ikisema kuwa kesho itakuwa Ijumaa ya Ghadhabu na fursa kwa ulimwengu wa Kiislamu kuonyesha hasira zao dhidi ya Washington na Tel Aviv.
-
Baraza la Usalama laitisha kikao cha dharura kuzungumzia Quds baada ya uchokozi wa Trump
Dec 07, 2017 03:59Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeitisha kikao cha dharura kesho Ijumaa kuzungumzia uamuzi wa rais wa Marekani, Donald Trump wa kuitangaza Baytul Muqaddas kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Iran yatoa jibu kwa uamuzi wa Marekani wa kuhamishia ubalozi wake Baitul Muqaddas
Dec 07, 2017 00:36Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa taarifa maalumu, ambayo mbali na kulaani kutangazwa Baitul Muqaddas kuwa mji mkuu wa utawala ghasibu wa Israel imesisitiza pia kwamba tangazo hilo lilotolewa na Rais Donald Trump wa Marekani ni ukiukaji wa wazi wa maazimio ya kimataifa.
-
Rais wa Iran asisitiza juu ya Waislamu kuwa macho na Ubeberu na Uzayuni
Dec 06, 2017 22:13Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya udharura wa Waiskamu kuwa macho na njama za maadui.
-
Nchi za Ulaya: Hatua ya Marekani dhidi ya Quds inatia wasiwasi
Dec 06, 2017 11:31Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Italia, Uingereza, Sweden na Ujerumani wamesema kuwa wana wasiwasi mkubwa na uamuzi wa upande mmoja wa Rais Donald Trump wa Marekani wa kuutambua rasmi mji wa Quds kama mji mkuu wa utawala wa Kizayuni.
-
Misri yamuonya Trump dhidi ya kuvuruga mambo Mashariki ya Kati
Dec 06, 2017 04:20Rais Abdulfattah al-Sisi wa Misri amemtahadharisha mwenzake wa Marekani Donald Trump dhidi ya kuhamishia ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv hadi mji mtukufu wa Quds, huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
-
Abbas amtahadharisha Trump kuhusu hatari ya kuhamishia ubalozi Quds
Dec 06, 2017 01:23Kiongozi wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amewasiliana na viongozi kadhaa wa kimataifa akiwemo Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis akiwahimiza kupinga mpango wa Rais Donald Trump wa Marekani wa kutaka kuhamishia ubalozi wa nchi hiyo katika mji mtakatifu wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.
-
Radiamali ya OIC kwa siasa za Rais Trump kuhusiana na Quds
Dec 05, 2017 10:03Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imemtahadharisha Rais Donald Trump wa Marekani kuhusiana na kuutambua mji wa Quds kama mji mkuu wa utawala haramu wa Israel.
-
PLO: Kuuhamishia Quds ubalozi wa Marekani ni 'busu la mauti'
Dec 05, 2017 04:31Mwakilishi wa Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) nchini Marekani ameonya kuhusu madhara ya mpango wa Washington wa kuuhamisha ubalozi wake mjini Tel Aviv na kuupeleka katika mji mtakatifu wa Quds.
-
Ismail Hania: Kadhia ya Quds ni sababu ya Waislamu kuungana
Dec 04, 2017 23:14Ismail Hania, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesisitiza kwamba, kadhia ya Quds ni sababu ya Waislamu kuungana na kwamba, suala hilo lipo katika orodha ya masuala ya Waislamu yanayopaswa kuzingatiwa na kupewa kipaumbele.