Ismail Hania: Kadhia ya Quds ni sababu ya Waislamu kuungana
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i37193-ismail_hania_kadhia_ya_quds_ni_sababu_ya_waislamu_kuungana
Ismail Hania, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesisitiza kwamba, kadhia ya Quds ni sababu ya Waislamu kuungana na kwamba, suala hilo lipo katika orodha ya masuala ya Waislamu yanayopaswa kuzingatiwa na kupewa kipaumbele.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 04, 2017 23:14 UTC
  • Ismail Hania: Kadhia ya Quds ni sababu ya Waislamu kuungana

Ismail Hania, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesisitiza kwamba, kadhia ya Quds ni sababu ya Waislamu kuungana na kwamba, suala hilo lipo katika orodha ya masuala ya Waislamu yanayopaswa kuzingatiwa na kupewa kipaumbele.

Ismail Hania amesema hayo katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki na kutahadharisha kuhusu hatari ya maamuzi ya Marekani ya kuuhamisha ubalozi wake mjini Tel Aviv na kuupeleka katika mji mtakatifu wa Quds. 

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS  amesema bayana kwamba, uamuzi huo wa Marekani ni hatari katika mitazamo miwili. Amesema, kwa upande mmoja uamuzi huo ni hatari kwani utapelekea utawala haramu wa Israel uwe na udhibiti kwa Quds na kuandaliwa uwanja wa mji huo kufanywa kuwa wa Kiyahudi.

Masjidul Aqswa inayopatikana katika mji wa Quds

Ismail Hania ameongeza kuwa, hatari ya pili  ni kwamba, uamuzi huo unahesabiwa kuwa ni sehemu ya njama chafu za makubaliano ya karne baada ya kufutwa malengo matukufu ya Palestina.

Kwa upande wake Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki sambamba na kuonyesha umuhimu mkubwa anoutoa kwa kadhia ya Quds na hamu yake ya kuwa na nafasi muhimuu katika harakati pana zenye lengo la kuukomboa mji huo mtakatifuu kutoka katika makucha ya Wazayuni maghasibuu amesema kuwa, atawaalika viongozi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu katika kikao maalumu kwa ajili ya kuchunguza na kuujadili uamuzi huo wa Marekani. Baadhi ya ripoti zinasema kuwa, Jumatano ya kesho, Donald Trump anakusudia kutangaza kuutambua rasmi mji wa Quds kuwa mji mkuu wa utawala pandikizi wa Israel.