Dec 06, 2017 15:01 UTC
  • Nchi za Ulaya: Hatua ya Marekani dhidi ya Quds inatia wasiwasi

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Italia, Uingereza, Sweden na Ujerumani wamesema kuwa wana wasiwasi mkubwa na uamuzi wa upande mmoja wa Rais Donald Trump wa Marekani wa kuutambua rasmi mji wa Quds kama mji mkuu wa utawala wa Kizayuni.

Anjelino Alfano Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia amesema kuwa Roma inatiwa wasiwasi na matukio yote na maamuzi yanayokinzana na maagizo ya jamii ya kimataifa kuhusu kadhia ya Palestina. 

Anjelino Alfano, Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia

Boris Johnson Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza pia leo Jumatano amebainisha wasiwasi wake kuhusu ripoti zinazotolewa kwamba kuna uwezekano Rais Trump akauhamishia ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv hadi katika mji wa Quds na kueleza kuwa nchi yake haina mpango wowote wa kuuhamishia ubalozi wake huko Quds. 

Boris Johnson, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza

Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani pia imetahadharisha kuhusu uamuzi wa Trump kuhusu kuutambua rasmi mji wa Quds kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni na kueleza kuwa hatua kama hiyo inaweza kuandaa uwanja wa kujiri machafuko katika ardhi nzima ya Palestina. Nayo Wizara ya Mambo ya Nje ya Sweden imeutaja umauzi huo wa Marekani kuwa ni maafa. Wakati huo huo Afisa mmoja wa Marekani amesema kuwa Rais Trump leo Jumatano anatazamiwa kutangaza azma yake hiyo ya kuuhamishia ubalozi wa nchi hiyo kutoka Tel Aviv hadi Quds kupitia hotuba atakayoitoa baadaye.

Tags