-
Tshisekedi aapishwa kuwa Rais mpya wa Congo DR + Sauti
Jan 24, 2019 12:27Kiongozi wa upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felix Tshisekedi amepishwa leo kushika hatamu za uongozi wa nchi hiyo akimrithi Rais Joseph Kabila aliyemaliza muda wake. Hatua hiyo inahesabiwa kuwa ya kwanza katika nchi hiyo ya katikati mwa Afrika ya kukabidhiana madaraka kwa njia ya amani na ya kidemokrasia katika kipindi hote cha miaka 59 iliyopita.
-
Hafla ya kumuapisha rais mpya wa Kongo DR yaakhirishwa
Jan 22, 2019 04:20Sherehe za kumuapisha rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zilizotazamiwa kufanyika leo Jumanne zimeakhirishwa na sasa zitafanyika baadaye wiki hii.
-
Rais Rouhani: Vita dhidi ya teknolojia na mabadiliko mapya, ni jambo la zamani sana
Jan 21, 2019 13:01Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, sekta ya mawasiliano na tekonolojia ya habari ni nembo ya mabadiliko ya jamii mbalimbali katika suala zima la ustawi wa kisayansi na kusisitiza kwamba, kuwa na welewa sahihi na kuamiliana kwa njia nzuri na uhakika huo, ndiyo njia pekee ya kuweza kudhibiti na kuzuia matatizo yanayotokana na maendeleo ya kiteknolojia.
-
Maandamano Zimbabwe baada ya ongezeko la bei ya mafuta kwa 150%
Jan 14, 2019 12:00Wananchi wa Zimbabwe hii leo wamefanya maandamano katika miji mikubwa ya nchi hiyo ukiwemo mji mkuu Harare, kulalamikia ongezeko la bei ya fueli kwa asilimia 150 lililotangazwa jana na Rais Emmerson Mnangagwa wa nchi hiyo.
-
Eneo la Puntland la Somalia lapata rais mpya
Jan 08, 2019 21:31Bunge la eneo lenye mamlaka ya ndani la Puntland limemchagua Said Abdullahi Deni kuwa rais eneo hilo, kuchukua nafasi ya Abdiweli Mohamed Ali Gaas.
-
Martin Fayulu, mgombea wa upinzani aongoza katika kura ya maoni DRC
Dec 28, 2018 12:34Utafiti mpya wa maoni umeonesha kuwa mgombea wa muungano wa upinzani wa Lamuka katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Martin Fayulu ndiye mwenye nafasi kubwa ya kuibuka mshindi katika uchaguzi wa rais unaotazamiwa kufanyika Jumapili ijayo.
-
Uchaguzi Madagascar; Ravalomanana apinga ushindi wa Rajoelina mahakamani
Dec 28, 2018 12:32Siku moja baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Madagascar kutangaza matokeo ya muda yaliyoonesha kuwa rais wa zamani wa nchi hiyo Andry Rajoelina ndiye aliyepata kura nyingi zaidi katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais iliyofanyika Disemba 19, mpinzani wake mkuu Marc Ravalomanana ameenda mahakamani kupinga matokeo hayo.
-
Mshauri wa Bashar al-Assad: Wamarekani wamekimbia Syria
Dec 23, 2018 23:20Mshauri wa kisiasa na wa masuala ya habari wa Rais wa Syria amesema kuhusu hatua ya wanajeshi wa Marekani kuondoka nchini humo kwamba: Wamarekani wamekimbia, kwa sababu sisi tumesimama imara.
-
Marais 2 wa zamani wajitangaza washindi wa duru ya pili ya uchaguzi Madagascar
Dec 20, 2018 11:28Wagombea wawili wa duru ya pili ya uchaguzi wa rais nchini Madagascar, ambao wamewahi kuwa marais wa kisiwa hicho, Marc Ravalomanana na Andry Rajoelina, wamejitangaza washindi wa uchaguzi huo uliofanyika jana, licha ya Tume ya Uchaguzi kusema kuwa imehesabu asilimia tano tu ya kura kufikia sasa.
-
Duru ya pili ya uchaguzi wa Rais Madagascar yafanyika leo, marais 2 wa zamani wachuana
Dec 19, 2018 04:06Wananchi wa Madagascar waliotimiza masharti ya kupiga kura mapema leo wameelekea katika masanduku ya kupigia kura kushiriki duru ya pili ya uchaguzi wa rais, unaowachuanisha marais wawili wa zamani wa kisiwa hicho, Marc Ravalomanana na Andry Rajoelina.