-
EAC yataka waasi wa M23 waondoke mara moja mashariki mwa DRC
Jun 21, 2022 03:32Jumuiya ya Afrika Mashariki imelitaka kundi la waasi la M23 liondoke mara moja katika mji wa Bunagana unaodhibitiwa na wanamgambo hao, huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
DRC yafunga mpaka na Rwanda baada ya askari wake kuuawa
Jun 18, 2022 07:57Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetangaza kufunga mpaka wake na Rwanda baada ya askari wa jeshi la DRC kuuawa kwa kupigwa risasi wakati jeshi hilo lilipowashambulia askari wanaolinda mpaka ndani ya ardhi ya Rwanda.
-
Kufuta Uingereza safari ya kwanza ya ndege ya kuwahamishia kwa lazima wakimbizi nchini Rwanda
Jun 16, 2022 21:47Katika hali ambayo, viongozi wa Uingereza wanang'ang'ania msimamo wao wa kuhamishia nchini Rwanda wakimbizi wanaoomba hifadhi nchini humo, safari ya kwanza ya ndege ambayo ilikusudiwa na Uingereza kuwasafirisha kwa lazima wakimbizi na kuwapeleka nchini Rwanda, imeakhirishwa.
-
Kwa mara nyingine, Iran yalaani jaribio la UK la kuwahamishia wakimbizi nchini Rwanda
Jun 15, 2022 03:01Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran kwa mara nyingine tena amelaani jaribio la Uingereza la kuwahamishia kwa lazima wakimbizi wa nchi hiyo huko Rwanda na kusema kuwa hiyo ni aibu ya kihistoria.
-
Uingereza yafuta safari ya kwanza ndege ya kuwahamishia kwa lazima wakimbizi nchini Rwanda
Jun 14, 2022 22:19Safari ya kwanza ya ndege ambayo ilikusudiwa na Uingereza kuwasafirisha kwa lazima wakimbizi na kuwapeleka nchini Rwanda, imeakhirishwa.
-
UNHCR: Sera ya Uingereza ya kuhamishia watafuta hifadhi Rwanda si sahihi
Jun 14, 2022 03:27Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR Filippo Grandi, ametupilia mbali uamuzi wa serikali ya Uingereza wa kuwahamishia Rwanda watafuta hifadhi wanaokwenda nchini humo huku akisema makubaliano hayo ya kando kati ya nchi mbili hizo ni makosa.
-
UN yajitenga na mpango wa kuwahamishia wakimbizi wa UK nchini Rwanda
Jun 11, 2022 05:50Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limejiweka mbali na madai kuwa linaunga mkono mpango wa kuwahamishia Rwanda wakimbizi na watu wanaotafuta hifadhi nchini Uingereza.
-
DRC yaituhumu Rwanda kuwa imetuma mamia ya askari nchini humo
Jun 09, 2022 18:51Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limedai kuwa Rwanda imetuma mamia ya askari ndani ya ardhi ya nchi hiyo, huku wasiwasi na taharuki ikiendelea kushuhudiwa kati ya nchi hizo jirani na kutishia uhusiano baina yao.
-
Rwanda : Awamu ya kwanza ya wahamiaji kutoka Uingereza watawasili hivi karibuni
May 20, 2022 03:00Waziri mkuu wa Rwanda, Edouard Ngirente, amesema awamu ya kwanza ya wahamiaji kutoka nchini Uingereza, watawasili huko Rwanda hivi karibuni, na kwamba nchi hiyo imekamilisha matayarisho ya kuwapokea.
-
Burundi: Uhusiano na Rwanda utaimarika zaidi ikitukabidhi wahusika wa jaribio la mapinduzi
May 15, 2022 03:36Rais Evariste Ndayishimiye wa Burundi, amesema uhusiano wa nchi yake na Rwanda utakuwa mzuri zaidi iwapo watu waliopanga na kufadhili jaribio la mapinduzi ya kijeshi ya 2015 wanaodhaniwa kuwa wako mafichoni jijini Kigali watarejeshwa mjini Gitega kufunguliwa mashtaka.