-
Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran asifu nafasi ya Ayatullah Hashimi Rafsanjani
Jan 13, 2017 10:35Khatibu wa Sala ya Ijumaa katika jiji la Tehran amesema kuwa marehemu Ayatullah Hashimi Rafsanjani alikuwa akiwafikiria vijana, akibainisha Uislamu wa kweli na Qur'ani Tukufu kabla na baada ya Mapinduzi ya Kiislamu.
-
Ayatullah Khatami: Harakati ya Dei 19 ilikuwa nembo ya umoja wa taifa la Iran
Jan 06, 2017 10:44Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, harakati ya Dei 19 iliyosadifiana na Januari 9 mwaka 1978 ulikuwa mwanzo wa hatua ya pili ya mapinduzi ya Kiislamu na nembo ya umoja wa taifa la Iran.
-
Khatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran aonya kuhusu jinai za Saudia, Bahrain
Dec 30, 2016 12:29Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran ameonya kuhusu mauaji na ukandamizaji unaofanywa na tawala za kikoo za Saudi Arabia na Bahrain dhidi ya mataifa ya Waislamu na kusema tawala hizo zinaelekea kusambaratika kutokana na jinai zao hizo.
-
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran apongeza kukombolewa mji wa Halab nchini Syria
Dec 16, 2016 11:30Khatibu wa Sala ya Ijumaa katika mji wa Tehran amesema kuwa wanajeshi wa Syria kwa kushirikiana na vikosi vya muqawama wameukomboa mji wa Halab yaani Aleppo uliokuwa ukishikiliwa na magaidi huko kaskazini mwa Syria na hivyo kuzima njama za maadui wa Uislamu.
-
Ijumaa tarehe 16 Disemba, 2016
Dec 16, 2016 01:50Leo ni ijumaa tarehe 16 Rabiul Awwal 1438 Hijria, sawa na Disemba 16, 2016.
-
Ayatullah Khatami: Iran itatoa jibu kali kwa ukwamishaji wa Marekani kuhusu JCPOA
Dec 09, 2016 10:40Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo hapa Tehran ameeleza kuwa jibu litakalotolewa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa njama na ukwamishaji unaofanywa na Marekani kuhusu Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA litakuwa kali.
-
'Iran itatoa jibu kali baada ya Marekani kukiuka mapatano ya nyuklia'
Dec 02, 2016 12:43Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran amesema hatua ya Bunge la Congress la Marekani kurefusha vikwazo dhidi ya Iran ni ukiukaji wa wazi wa mapatano ya nyuklia baina ya Iran na madola sita makubwa duniani.
-
Utawala wa Aal Khalifa waendelea kuzuia Sala ya Ijumaa nchini Bahrain
Dec 02, 2016 12:09Utawala wa ukoo wa Aal Khalifa nchini Bahrain, kwa wiki ya 25 mfululizo, umewazuia Waislamu kusali Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Imam Sadiq AS magharibi mwa mji mkuu Manama.
-
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran alaani shambulio la kigaidi dhidi ya Mazuwwar nchini Iraq
Nov 25, 2016 11:49Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amelaani vikali shambulio la jana la kigaidi mjini Hilla Iraq lililopelekea kuuawa shahidi zaidi ya wafanyaziara 80 wa Imam Hussein as wakiwemo Mazuwwar 40 wa Kiirani.
-
Ayatullah Kashani: Hamasa ya Arubaini ya Imam Hussein ni ishara ya muqawama wa Waislamu
Nov 18, 2016 11:39Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, hamasa ya Arubaini ya Imam Hussein (as) mjukuu wa Mtume Muhammad (saw), ni ishara ya muqawama wa Waislamu wa dunia, hususan wa madhehebu ya Kishia na Kisuni dhidi ya adui wa Uislamu.