Utawala wa Aal Khalifa waendelea kuzuia Sala ya Ijumaa nchini Bahrain
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i20605-utawala_wa_aal_khalifa_waendelea_kuzuia_sala_ya_ijumaa_nchini_bahrain
Utawala wa ukoo wa Aal Khalifa nchini Bahrain, kwa wiki ya 25 mfululizo, umewazuia Waislamu kusali Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Imam Sadiq AS magharibi mwa mji mkuu Manama.
(last modified 2026-03-03T12:46:59+00:00 )
Dec 02, 2016 12:09 UTC
  • Utawala wa Aal Khalifa waendelea kuzuia Sala ya Ijumaa nchini Bahrain

Utawala wa ukoo wa Aal Khalifa nchini Bahrain, kwa wiki ya 25 mfululizo, umewazuia Waislamu kusali Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Imam Sadiq AS magharibi mwa mji mkuu Manama.

Ijumaa ya leo, baada ya waandamanaji kuketi mbele ya nyumba ya Sheikh Issa Qassim, mwanazuoni wa Kishia aliye katika kifungo cha nyumbani katika eneo la Ad Diraz magharibi mwa Manama, wanajeshi wa utawala wa Aal Khalifa walisambaza magari kadhaa na kufunga njia inayotumiwa na waumini kuelekea eneo hilo na hivyo kuzuia kusaliwa Sala kubwa zaidi ya Ijumaa nchini humo.

Wapinzani wa ukoo wa Aal Khalifa nchini Bahrain wanalalamikia kuanza tena kesi ya mwanazuoni huyo wa ngazi za juu wa Kishia kwa msingi huo wamefanya maandamano makubwa leo na yanatazamiwa kuendelea kesho.

Aidha wapinzani nchini Bahrain wamesistiiza kuendeleza maandamano ya amani kupinga kesi ya Sheikh Ali Salman kiongozi wa chama cha Kiislamu cha Al Wifaq. Waandamanaji pia wanataka wafungwa 40,000 wa kisiasa nchini humo waachiliwe huru.

Sheikh Issa Qassim

Wapinzani wa utawala wa Bahrain waishio nje ya nchi pia wamemtaka Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May atumie ushawishi wake katika ukoo wa Aal Khalifa na autake usitishe hujuma dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia. May anatazamiwa kutembelea Bahrain hivi karibuni kushiriki katika kikao cha Baraza la Ushirikinao la Ghuba ya Uajemi.

Ikumbukwe kuwa, Bahrain imekuwa ikishuhudia maandamano ya amani ya wananchi wanaopinga utawala wa Aal Khalifa tangu Februari mwaka 2011. Matakwa makuu ya wananchi hao ni kuwepo utawala wa kisheria, kukomeshwa ubaguzi wa kimadhehebu, kufanyika mageuzi ya kisiasa na kuheshimiwa haki za binadamu.

Baadhi ya ripoti zinaonyesha kuwa, maelfu ya wananchi wa Bahrain wanashikiliwa jela na katika korokoro za nchi hiyo huku 150 wakiwa wamehukumiwa vifungo vya maisha jela.