Dec 16, 2016 05:20 UTC
  • Ijumaa tarehe 16 Disemba, 2016

Leo ni ijumaa tarehe 16 Rabiul Awwal 1438 Hijria, sawa na Disemba 16, 2016.

Siku kama ya leo miaka 1437 Hijria kwa mujibu wa baadhi ya mapokezi ya historia, Swala ya kwanza ya Ijumaa iliswaliwa na Mtume Muhammad (saw) baada ya mtukufu huyo kuhama mji wa Makka. Baada ya kuwasili katika eneo la Bani Salim bin Auf kwa jina la Quba karibu na Madina wakati wa adhuhuri, Mtume (saw) alitoa hotuba na kusimamisha Swala ya Ijumaa mahala hapo. Wanahistoria wanasema hiyo ilikuwa Swala ya kwanza ya Ijumaa katika Uislamu. Hatua hiyo pia inaonesha umuhimu wa ibada hiyo ya kiroho na kisiasa ambayo Bwana Mtume aliamua kuitekeleza mara tu baada ya kuwasili karibu na mji wa Madina. 

نماز جمعه

Miaka 66 iliyopita katika siku kama ya leo ilianza harakati ya kupigania uhuru ya watu wa Cyprus kwa shabaha ya kuhitimisha ukoloni wa Waingereza kisiwani humo. Kisiwa cha Cyprus kilichoko katika Bahari ya Miditerranean kiliwekwa chini ya utawala wa Kiothmania katika karne ya 16. Mwaka 1925 Uingereza ilikiunganisha kisiwa hicho na makoloni yake na tangu wakati huo kulitokea mapigano baina wakazi wa kisiwa hicho yaani Waturuki na Wagiriki. Hatimaye Cyprus ilipata uhuru mwaka 1974 baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa na Wagiriki huku Waturuki wa kisiwa hicho wakidhibiti eneo la kaskazini la nchi hiyo. 

Cyprus

Siku kama ya leo miaka 25 iliyopita mwili wa Mhandisi Muhammad Jawad Tundguyan, waziri wa mafuta wa wakati huo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ulirejeshwa nchini Iran kutoka Iraq baada ya kupita miaka 11. Waziri Tundguyan na maafisa wengine kadhaa wa wizara hiyo walitekwa nyara na wanajeshi wavamizi wa Iraq wakati walipokuwa katika ziara ya kutembelea visima vya mafuta vya kusini mwa Iran. Waziri huyo na wenzake walitekwa nyara mwezi mmoja baada ya Iraq kuvamia ardhi ya Iran. Utawala wa Saddam wakati huo uliendelea kukanusha kutekwa nyara Mhandisi Tundguyan kwa muda fulani, lakini hatimaye ulikiri kumteka nyara waziri huyo wa zamani wa mafuta wa Iran. Uchunguzi wa kidaktari na ushahidi uliotolewa na watu waliokuwa karibu na Waziri Muhammad Jawad Tundguyan ulithibitisha kwamba waziri huyo wa zamani wa mafuta wa Iran alikufa shahidi kutokana na kuteswa vikali na askari jeshi wa utawala wa Baath wa Iraq.

Mhandisi Muhammad Jawad Tundguyan

Siku kama hii ya leo miaka 18 iliyopita Mahakama ya Rufaa ya Paris ilimhukumu kifungo na kumtoza faini mwanafalsafa na msomi mashuhuri wa nchi hiyo, Roger Garaudy, kwa kosa eti la kukana jinai dhidi ya binadamu katika kitabu chake cha 'The Founding Myths of Israeli Politics'. Katika kitabu hicho msomi huyo Mfaransa alithibitisha kisayansi na kwa hoja madhubuti kwamba Wazayuni walishirikiana na Manazi katika Vita vya Pili vya Dunia. Vilevile amethibitisha kwa hoja na ushahidi kwamba, kwa shabaha ya kutaka kupata uungaji mkono wa kuunda dola bandia la Israel katika ardhi ya Palestina, Wazayuni walikuza na kutia chumvi kupita kiasi jinai zilizofanywa na Adolph Hitler dhidi ya Mayahudi. Katika kitabu cha 'The Founding Myths of Israeli Politics' Profesa Garaudy anasema, idadi ya Mayahudi milioni 6 inayotajwa na Wazayuni kuwa iliuawa na Wajerumani wa zama za Hitler imetiwa chumvi kupita kiasi kwani jamii ya Wayahudi katika kipindi hicho haikuwa kubwa kiasi hicho. Msomi huyo alikamatwa na kuhukumiwa kifungo nchini Ufaransa kutokana na maoni yake, suala ambalo limethibitisha urongo wa madai ya demokrasia na uhuru wa maoni nchini Ufaransa.

Mwanafalsafa wa Ufaransa, Roger Garaudy

 

Tags