-
Saudia imeshindwa katika vita dhidi ya Yemen
Feb 16, 2020 07:30Kuvunjika makubaliano ya Riyadh, kuondoka kikamilifu askari wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) kutoka Yemen na kutunguliwa ndege ya kivita aina ya Tornado ya muungano vamizi wa Saudia, kabla ya jambo lolote lile, ni mambo yanayoashiria kushindwa serikali ya Riyadh katika vita vyake vya kichokozi dhidi ya Yemen.
-
Libya: Misri, Saudia, Imarati zinavunja azimio la Baraza la Usalama
Dec 20, 2019 23:34Mwakilishi wa serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, nchi za Misri, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) zinavunja azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa uungaji mkono wao kwa jenerali muasi, Khalifa Haftar.
-
Afrika Kusini yasitisha uuzaji silaha kwa Saudia, UAE
Nov 23, 2019 08:27Afrika Kusini imetangaza kuwa inasitisha uuzaji wa silaha zake kwa Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) baada ya kubainika kuwa tawala hizo mbili zinawakabidhi wanamgambo wa Yemen baadhi ya silaha hizo na hivyo kukiuka mapatano ambayo yanazuia silaha zilizonunuliwa kutoka Afrika Kusini kufikia pande za tatu.
-
Abdul-Malik al-Houthi: Saudia na waitifaki wake wasubiri matokeo mabaya ya uvamizi wao
Nov 10, 2019 04:22Kiongozi wa wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen ameuonya vikali muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya nchi hiyo na kusisitiza kuwa, wavamizi hao wataendelea kuandamwa na vipigo na wajiandae kwa matokeo mabaya ya uvamizi wao.
-
Kuwait yazifikishia Saudia na Bahrain ujumbe wa amani kutoka Iran
Nov 06, 2019 04:25Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait Khaled al-Jarallah amesema nchi yake imezifikishia Saudi Arabia na Bahrain ujumbe wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wa kutaka amani katika eneo la Ghuba ya Uajemi.
-
Shutuma na lawama za Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki kwa Saudia na Imarati
Nov 01, 2019 04:18Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Mevlüt Çavuşoğlu amezikosoa na kuzilaumu Saudi Arabia na Imarati kwa sababu ya kadhia tofauti za eneo na kimataifa na akasisitiza kwamba Saudia inapasa iwajibishwe kwa kuishambulia kijeshi Yemen.
-
Mamia ya raia wa Ethiopia waondoka Saudia Arabia
Oct 26, 2019 23:09Serikali ya Ethiopia imewaondoa mamia ya raia wake kutoka Saudi Arabia katika kipindi cha wiki za hivi karibuni.
-
Watu sita watiwa mbaroni Saudia kwa kumkosoa mpambe wa Bin Salman
Oct 25, 2019 23:05Wanaharakati wa haki za binaadamu nchini Saudia wameripoti habari ya kutiwa mbaroni na maafisa usalama wa nchi hiyo watu sita, kwa tuhuma ya kumkosoa mmoja wa watu wa karibu na Mohammad Bin Salman, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa nchi hiyo.
-
Wapalestina waliotiwa mbaroni Saudia wakabiliwa na mateso
Oct 21, 2019 23:50Mwanachama wa ngazi ya juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema kuwa raia wa Palestina waliokamatwa nchini Saudi Arabia wanakabiliwa na mateso mbalimbali.
-
Larijani: Marekani ndiye mchochezi mkuu wa uhasama kati ya Iran na Saudia
Oct 16, 2019 01:06Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu haina tatizo lolote wala haipingi mpango wowote wa kupatiwa ufumbuzi mikwaruzano na uhasama uliopo kati yake na Saudi Arabia, lakini Marekani ndiyo kizingiti kikuu katika kuafikiwa jambo hilo.