-
Waislamu milioni 1.4 wameshawasili Saudia kutekeleza Ibada ya Hija
Aug 25, 2017 03:14Zaidi ya Waislamu milioni 1.4 wameshawasili Saudi Arabia hadi hivi sasa kwa ajili ya kutekeleza ibada ya kila mwaka ya Hija ambayo inaanza wiki ijayo.
-
Raia 35 wauawa katika mashambulio ya kijeshi ya Saudia nchini Yemen
Aug 23, 2017 09:32Kwa akali watu 35 wameuawa nchini Yemen na makumi ya wengine kujeruhiwa kufuatia mashambulio ya anga ya ndege za kijeshi za utawala vamizi wa Saudi Arabia katika mji mkuu Sana'a.
-
Makumi ya watu wauawa Yemen katika shambulio la anga la Saudia dhidi ya maeneo ya raia
Aug 23, 2017 03:35Watu wasiopungua 30 wameripotiwa kuuawa katika mashambulio yaliyofanywa na ndege za kivita za utawala vamizi wa Saudi Arabia katika eneo la makaazi ya raia katika mkoa wa Sana'a mji mkuu wa Yemen.
-
Zarif: Iran inakaribisha kubadilika sera za kieneo za Saudi Arabia
Aug 23, 2017 03:13Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema: Ikiwa Saudi Arabia itaangalia upya siasa na sera zake za eneo la Mashariki ya Kati itapata jibu na radiamali chanya ya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Qatar: Tunaishitaki Saudia kwa kutishia kushambulia ndege zetu za abiria
Aug 21, 2017 03:53Serikali ya Qatar imetangaza kuwa imekusudia kuishitaki Saudi Arabia katika Umoja wa Mataifa kutokana na nchi hiyo kutishia kuzishambulia ndege zake za abiria.
-
Qatar yafichua nyaraka za uungaji mkono wa Saudia na Imarati kwa magaidi wa Al-Qaeda nchini Yemen
Aug 20, 2017 21:57Qatar imefichua nyaraka zinazoonyesha kuwa Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) zinawaunga mkono magaidi wa mtandao wa Al-Qaeda na kundi la kitakfiri la Daesh (ISIS) nchini Yemen.
-
Chuo Kikuu cha Queen Mary: Saudia inaeneza kipindupindu Yemen
Aug 19, 2017 23:52Utafiti uliofanywa na taasisi moja ya Uingereza umebaini kuwa, muungano unaoongozwa na Saudi Arabia katika vita dhidi ya watu wa Yemen ndio unaohusika na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu nchini Yemen kwa kuzuia misaada ya kibinadamu na kuyazingira maeneo yaliyokumbwa na ugonjwa huo.
-
Vita vya Saudi Arabia dhidi ya watoto wa Yemen
Aug 19, 2017 04:40Utangulizi wa ripoti iliyotayarishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres kuhusu ukiukwaji wa haki za watoto katika migogoro ya vita umeutuhumu muungano vamizi dhidi ya Yemen unaoongozwa na Saudi Arabia kuwa umekiuka haki za watoto.
-
UN: Hujuma za Saudi zimesababisha nusu ya vifo vya watoto Yemen
Aug 18, 2017 03:38Umoja wa Mataifa umesema asilimia 51 ya vifo na majeraha ya watoto wadogo nchini Yemen mwaka uliopita, yamesababishwa na mashambulio ya anga yanayofanywa na ndege za muungano wa kijeshi unaoongozwa na utawala vamizi wa Saudi Arabia dhidi ya nchi hiyo maskini jirani yake.
-
Askari wa Saudia waharibu kikamilifu eneo la al-Masoorah la mji wa Al-Awamiyah
Aug 16, 2017 22:08Viongozi wa utawala wa kidikteta wa Saudia Arabia wametangaza kuharibiwa kikamilifu eneo la Waislamu wa madhehebu ya Shia la al-Masoorah katika mji wa Al-Awamiyah jimbo la Qatif nchini Saudia.