-
UN yasikitishwa na uvunjaji wa haki za binadamu nchini Sudan
Dec 11, 2021 04:41Timu ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan imeelezea kusikishwa kwake na kuongezeka vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu nchini humo.
-
Al Burhan: Jeshi la Sudan litaacha siasa baada ya uchaguzi wa 2023
Dec 05, 2021 02:49Mkuu wa jeshi la Sudan, Abdel Fattah Al-Burhan, amesema kwamba jeshi litaondoka kwenye uwanja wa siasa baada ya uchaguzi uliopangwa kufanyika 2023, na kuongeza kuwa kuna "ishara nzuri" zinazohusiana na uungaji mkono mpya wa jamii ya kimataifa kwa Khartoum.
-
Radiamali ya Guterres kuhusu kupinga Wasudani kuwepo wanajeshi madarakani
Dec 02, 2021 08:44Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewataka Wasudani kuwa na busara na kuafiki mapatano yaliyosainiwa kati ya Waziri Mkuu na jeshi la nchi hiyo kwa lengo la kudhamini kipindi cha amani cha mpito kuelekea kuundwa serikali ya kiraia huko Sudan.
-
Wasudan waandamana kupinga utawala wa wanajeshi
Dec 01, 2021 04:51Wananchi wa Sudan wangali wanaendeleza maandamano ya kupinga mapatano ya kisiasa yaliyofikiwa karibuni kati ya wanajeshi na Abdalla Hamdok, ili kumrejesha kiongozi huyo katika nafasi yake ya Waziri Mkuu.
-
Kuendelea maandamano ya Wasudan mjini Khartoum
Nov 30, 2021 08:28Wananchi wa Sudan wanaendelea kufanya maandamano kulalamikia mapatano ya kisiasa yaliyofikiwa nchini humo pamoja na kutaka serikali ya kiraia iundwe haraka nchini.
-
Waziri Mkuu wa Sudan awatimua wakuu wa jeshi la Polisi
Nov 28, 2021 04:15Waziri Mkuu wa Sudan Abdallah Hamdok amewauzulu wakuu wa jeshi la Polisi baada ya watu zaidi ya 40 kuuawa katika ukandamizaji uliofanywa na jeshi hilo kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya mwezi uliopita yaliyopelekea Hamdok mwenyewe kuondolewa madarakani.
-
Askari wasiopungua sita wa Sudan wauawa katika mapigano ya mpakani na Ethiopia
Nov 28, 2021 00:05Jeshi la Sudan limesema, askari wake kadhaa wameuawa katika shambulio lililofanywa na vikosi vya jeshi la Ethiopia katika eneo la mpakani linalozozaniwa na nchi mbili.
-
Viongozi wa kisiasa waachiwa huru Sudan baada ya kufanya mgomo wa kususia kula
Nov 27, 2021 09:02Wizara ya habari ya Sudan imetangaza kuwa, maafisa kadhaa wa kisiasa wa nchi hiyo wameachiwa huru kutoka jela walizokuwa wakishikiliwa baada ya kufanya mgomo wa kususia kula.
-
Wasudan washinikiza wanajeshi warudi makambini, kuundwe serikali ya raia
Nov 25, 2021 23:18Wananchi wa Sudan wameendelea na maandamano yao wakishinikiza wanajeshi warudi makambini ili waruhusu kuundwa serikali ya kiraia na ya kidemokrasia nchini humo.
-
Kuendelea mgogoro huko Sudan
Nov 24, 2021 22:58Licha ya kufikiwa mapatano ya kisiasa kati ya Abdel Fattah al Burhan Kamanda Mkuu wa Jeshi la Sudan na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Abdallah Hamdok na kisha Waziri Mkuu huyo kurejeshwa madarakani, baadhi ya vyama vya kisiasa na akthari ya raia wa nchi hiyo wamepinga mapatano hayo na kumtuhumu Hamdok kuwa amewasaliti.