-
Sudan inahitaji dola bilioni 5 kusaidia bajeti ya nchi
Nov 08, 2019 23:44Waziri wa Fedha wa Sudan amesema kuwa nchi hiyo inahitaji kiasi cha dola zipatazo bilioni 5 ili kusaidia bajeti ya nchi na hivyo kuzuia kuporomoka uchumi wa nchi na kusaidia kutekelezwa marekebisho mbalimbali baada ya kupinduliwa mtawala wa zamani wa nchi hiyo, Omar al Bashir.
-
Sudan yazindua satalaiti yake ya kwanza iliyounda kwa ushirikiano na China
Nov 06, 2019 11:56Sudan imezindua kwa kurusha angani satalaiti yake ya kwanza itakayoshughulika na utafiti wa kijeshi, kiuchumi na wa tekonolojia ya anga za mbali. Akizungumza katika kikao na maafisa waandamizi wa usalama, mkuu wa Baraza Kuu la Utawala la Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan ametangaza kuwa, satalaiti hiyo imetengezwa kwa ushirikiano na Jamhuri ya Watu wa China.
-
Njama za Saudia na Imarati za kusambaratisha mapinduzi ya Sudan zalalamikiwa
Nov 02, 2019 23:03Chama cha Kikomonisti cha Sudan kimezituhumu Saudi Arabia na Imarati kwamba, zinafanya njama za kusambaratisha mapinduzi ya wananchi wa nchi hiyo yaliyomuondoa madarakani aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Omar Hassan al-Bashir.
-
Baraza la Usalama la UN laafiki kurefushwa muda wa kuhudumu UNAMID katika eneo la Darfur, Sudan
Nov 01, 2019 03:49Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeafiki kurefushwa muda wa kuhudumu kikosi cha pamoja cha askari wa kulinda amani wa umoja huo na wale wa Umoja wa Afrika kinachojulikana kama UNAMID katika eneo la Darfur, magharibi mwa Sudan.
-
Askari elfu 10 wa Sudan waondoka Yemen
Oct 31, 2019 07:04Naibu Mkuu wa Baraza la Utawala wa Mpito nchini Sudan amesema kuwa askari elfu 10 wa nchi hiyo wameondoka nchini Yemen.
-
Al Bashir abambwa akiwa na simu ya kisasa ndani ya jela Sudan
Oct 27, 2019 04:03Kugunduliwa simu ya kisasa ya rais aliyeondolewa madarakani na wananchi wa Sudan akiwa katika jela kumezusha malalamiko makubwa nchini humo.
-
Maelfu waandamana Sudan wakitaka kuvunjwa chama cha al-Bashir
Oct 22, 2019 04:36Maelfu ya wananchi wa Sudan wamejitokeza mabarabarani katika maandamano ya kushinikiza kuvunjiliwa mbali kilichokuwa chama tawala nchini humo.
-
Sudan yasema waasi wa Darfur wamekiuka mapatano ya amani
Oct 21, 2019 04:45Jeshi la Sudan limesema kundi la waasi la SLM limekiuka mapatano ya kusitisha vita yaliyotangazwa baina ya pande hasimu nchini humo.
-
Mazungumzo ya serikali ya Sudan na waasi yaanza Juba
Oct 15, 2019 09:44Wawakilishi wa serikali ya Sudan na viongozi wa makundi ya waasi wanaendeleza mazungumzo katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba.
-
Sadiq al-Mahdi: Serikali ya Mpito ya Sudan inakabiliwa na changamoto ambazo huenda zikaisambaratisha
Oct 12, 2019 22:55Sadiq al-Mahdi, kiongozi wa Hizb al-Umma al-Qawmmy amesema kuwa, Serikali ya Mpito ya Sudan inakabiliwa na changamoto ambazo kama itashindwa kuzipatia ufumbuzi basi itakuwa imejichimbia kaburi.