-
Wawakilishi wa Baraza la Kijeshi Sudan na muungano wa upinzani wasaini makubaliano ya kisiasa
Jul 17, 2019 08:48Wawakilishi wa Baraza la Kijeshi la uongozi wa mpito nchini Sudan na muungano wa upinzani leo Jumatano wamesaini makubaliano ya kisiasa kama sehemu ya kugawana madaraka kwa lengo la kuielekeza nchi hiyo kwenye demokrasia.
-
Wapinzani Sudan: Wanajeshi wasipewe kinga ya kushtakiwa
Jul 17, 2019 03:02Muungano mkuu wa upinzani nchini Sudan umepinga vikali mpango wa kuwapa wanajeshi wa nchi hiyo kinga mutlaki ya kushtakiwa, ukisisitiza kuwa waliohusika na vitendo vya jinai wanapaswa kubebeshwa dhima.
-
Mkutano wa Baraza la Kijeshi la Sudan na kambi ya upinzani waakhirishwa
Jul 15, 2019 05:54Muungano wa Uhuru na Mabadiliko nchini Sudan umetangaza kuwa, mkutano uliokuwa umepangwa kufanyika leo na wawakilishi wa Baraza la Kijeshi linalotawala nchi hiyo chini ya upatanishi wa Ethiopia na Umoja wa Afrika umeakhirishwa hadi Jumanne ya kesho.
-
Mjumbe wa AU: Pande hasimu Sudan kusaini makubaliano ya kisiasa leo
Jul 12, 2019 20:39Wawakilishi wa Baraza la Kijeshi la Mpito nchini Sudan na muungano wa upinzani wa Uhuru na Mabadiliko wanatazamiwa kusaini makubaliano ya kisiasa leo Jumamosi, saa chache baada ya jeshi hilo kutangaza kuwa limezima jaribio la mapinduzi.
-
Baraza la Kijeshi la Uongozi Sudan latangaza kuzima jaribio la mapinduzi dhidi yake
Jul 11, 2019 22:41Baraza la Kijeshi la Uongozi wa mpito Sudan limezima jaribio la mapinduzi dhidi yake. Hayo yameelezwa kupitia taarifa iliyotangazwa jana na jenerali wa ngazi ya juu kupitia televisheni ya nchi hiyo. Amesema kuwa maafisa 12 na wanajeshi 4 wametiwa mbaroni.
-
UN yatilia mkazo udharura wa kuanza tena mazungumzo ya amani Sudan
Jul 10, 2019 08:22Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kuanza tena mazungumzo baina ya wapinzani na watawala wa kijeshi nchini Sudan.
-
Baraza la Kijeshi Sudan: Tuko tayari kukabidhi muswada wa makubaliano na wapinzani
Jul 10, 2019 03:28Baraza la Kijeshi la Sudan limesema kuwa, liko tayari kukabidhi muswada wa makubaliano yaliyofikiwa baina ya baraza hilo na makundi mbalimbali ya wapinzani.
-
Answarullah: Wasudan waondokane na ubeberu wa Saudia na Imarati
Jul 09, 2019 22:05Mjumbe wa Baraza la Kisiasa la Harakati ya Wananchi ya Answarullah nchini Yemen amesema kuwa, raia wa Sudan na nchi yao wanatakiwa kuwa huru mbele ya udhibiti wa vibaraka wa Saudia na Imarati.
-
Al Burhan: Kumefanyika majaribio kadhaa ya mapinduzi Sudan
Jul 08, 2019 06:26Mkuu wa Baraza la Kijeshi linalotawala Sudan amesema kuwa jeshi la nchi hiyo imezima majaribio kadhaa ya mapinduzi.
-
Sisitizo la kutekelezwa makubaliano ya kugawana madaraka Sudan
Jul 08, 2019 02:07Mkuu wa Baraza la Kijeshi la Mpito la Sudan ameahidi kwamba, baraza hilo litatekeleza kikamilifu makubaliano yaliyofikiwa kati yake na Muungano wa Uhuru na Mageuzi na kwamba, linaunga mkono makubaliano hayo.