-
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lafanya kikao cha dharura kujadili mgogoro wa Sudan
Jun 05, 2019 03:37Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limefanya kikao cha dharura na kisicho cha wazi kujadili hali ya mambo nchini Sudan.
-
Mkuu wa Mkoa wa Khartoum, Sudan ajiuzulu katika kulaani mauaji ya raia
Jun 05, 2019 03:24Mkuu wa Mkoa wa Khartoum nchini Sudan, amejiuzulu nafasi yake hiyo katika kupinga na kulaani amri iliyotolewa na Baraza la Kijeshi la nchi hiyo ya kuwaua raia wanaoandamana.
-
Rais wa zamani wa Tunisia: Pembe tatu za shari za Kiarabu zimehusika na mauaji ya raia Sudan
Jun 04, 2019 23:28Rais wa zamani wa Tunisia amesema kuwa Baraza la Kijeshi linaloongoza Sudan limeua makumi ya raia wa nchi hiyo kwa amri ya pembetatu za shari ambazo ni Saudi Arabia, Imarati na Misri.
-
Iran yaliasa jeshi la Sudan likabidhi madaraka kwa raia
Jun 04, 2019 09:05Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kueleza kusikitishwa kwake na machafuko ya kisiasa nchini Sudan, imetoa mwito kwa Baraza la Mpito la Kijeshi kukabidhi madaraka kwa raia kama wanayoshinikiza wananachi wanaoandamana kwa miezi kadhaa sasa.
-
Wapinzani nchini Sudan wapinga mpango wa jeshi wa kukabidhi madaraka
Jun 04, 2019 09:00Wapinzani nchini Sudan wametangaza kuwa wanapinga mpango wa kukabidhi madaraka uliotangazwa na Baraza la Mpito la Kijeshi lililotwaa madaraka ya nchi baada ya kujiri maandamano yaliyompindua rais Omar al Bashir wa nchi hiyo mwezi Aprili mwaka huu.
-
Jeshi Sudan latangaza uchaguzi mkuu; mauaji ya waandamanaji yazidi kulaaniwa
Jun 04, 2019 02:22Jeshi nchini Sudan leo limetangaza kuvunja makubaliano yote ya kukabidhi madaraka kwa serikali ya mpito ya kiraia na badala yake limetangaza uchaguzi mkuu katika kipindi cha miezi tisa ijayo. Hayo yamekuja baada ya wanajeshi kushambulia waandamanaji na kuua raia 30 na kujeruhi mamia ya wengine jana Jumatatu.
-
Wapinzani Sudan wataka kuvunjwa Baraza la Kijeshi
Jun 03, 2019 21:51Muungano wa Uhuru na Mabadiko unaoundwa na vyama vya upinzani nchini Sudan umetoa wito wa kuvunjwa Baraza la Kijeshi linaloongoza nchi hiyo.
-
IGAD yasisitiza kuhusu usalama wa kipindi cha mpito Sudan Kusini
Jun 03, 2019 03:48Shirika la Kiserikali la Ustawi wa nchi za Mashariki mwa Afrika (IGAD) limezihimiza pande zote za Sudan Kusini kushiriki kikamilifu katika mpango wa mpito wa usalama ili kusaidia utekelezwaji wa mapatano mapya ya amani kwa wakati.
-
5 wauawa baada ya maafisa usalama kushambulia waandamanaji Sudan
Jun 03, 2019 02:44Habari kutoka Khartoum, mji mkuu wa Sudan zinaarifu kuwa, kwa akali watu watano wameuawa baada ya maafisa usalama nchini humo kushambulia kwa risasi hai maandamano ya wananchi wanaolalamikia hatua ya jeshi la nchi hiyo kung'ang'ania madaraka.
-
Kufungwa ofisi ya televisheni ya al Jazeera nchini Sudan
May 31, 2019 03:27Viongozi wa Sudan wameagiza kusimamishwa shughuli za televisheni ya al Jazeera nchini humo.