Arab League yapinga uingiliaji wa nchi ajinabi katika mgogoro wa Sudan
(last modified Tue, 18 Jun 2019 02:28:00 GMT )
Jun 18, 2019 02:28 UTC
  • Arab League yapinga uingiliaji wa nchi ajinabi katika mgogoro wa Sudan

Akiwa ziarani nchini Sudan Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) amesisitiza kuwa mgogoro wa Sudan unapasa kupatiwa ufumbuzi bila ya uingiliaji wa nchi yoyote ajinabi.

Ahmed Abul Gheit amefanya ziara nchini Sudan na kufanya mazungumzo na Abdul Fattah al Burhan Mkuu wa Baraza la Kijeshi la Uongozi wa Mpito la nchi hiyo na baadhi ya shakhsia wa nchi hiyo. Katika ziara hiyo huku akiliunga mkono Baraza la Kijeshi linaloongoza hivi sasa huko Sudan, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu amedai kuwa umoja huo unaunga mkono kukabidhiwa madaraka raia kwa njia ya amani na kutaka kupatiwa ufumbuzi mgogoro wa nchi hiyo bila ya uingiliaji wa nchi ajinabi. 

Ahmed Abul Gheit amesema kuwa ufumbuzi wa mgogoro wa sasa wa Sudan unapasa kuwa mahsusi kikamilifu kwa nchi hiyo na katika fremu ya kitaifa na mbali na uingiliaji wa nchi ajinabi; na kwa njia hiyo uhuru, kujitawala na matakwa ya matabaka ya wananchi wote wa Sudan yaweza kuheshimiwa. Baraza la Kijeshi la Uingozi wa Mpito la nchi hiyo linaungwa mkono na Saudi Arabia na Imarati. 

Mkuu wa baraza la kijeshi la mpito la Sudan katika mazungumzo na mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudia
 

Jeshi la Sudan tarehe tatu mwezi huu liliushambulia umati wa watu waliokuwa wamekusanyika mbele ya makao makuu ya jeshi huko Khartoum na kuuwa 118 kati yao.