-
Rais al Bashir: Sudan itauvuka mgogoro wa sasa
Dec 30, 2018 23:36Rais wa Sudan ameahidi kuwa nchi hiyo itaondokana na mgogoro unaosibu hivi sasa licha ya kuwepo pande zinazopambana na Sudan.
-
Uchunguzi: Umiliki wa silaha raia nchini Kenya wapiku wa polisi na wa wanajeshi
Dec 29, 2018 23:51Serikali ya Kenya inafanya juhudi za kuwashawishi watu wanaomiliki silaha bila kibali kukabidhi silaha zao lakini juhudi za huko nyuma zimefeli kwa sababu kumiliki silaha hivi sasa imekuwa ni sehemu katika maisha ya kila siku nchini humo.
-
Umoja wa Mataifa wataka kufanyike uchunguzi kuhusu mauaji ya waandamanaji Sudan
Dec 29, 2018 12:53Umoja wa Mataifa umelezea kusikitishwa sana na machafuko pamoja na mauaji ya waandamanaji nchini Sudan na umewataka viongozi wa nchi hiyo wafanye uchunguzi unaotakiwa wa kubaini kwa nini waandamanaji wanauawa.
-
Polisi Sudan wawashambulia waandamanaji wakitoka msikitini
Dec 28, 2018 12:37Maafisa usalama nchini Sudan wamewashambulia kwa mabomu ya kutoa machozi, waumini wa Kiislamu waliokuwa wakishiriki 'maandamano ya amani' baada ya Sala ya Ijumaa, katika mji wa Omdurman, nje kidogo ya mji mkuu Khartoum.
-
Waandishi wa habari nao waitisha mgomo nchini Sudan, Misri yamuunga mkono al Bashir
Dec 28, 2018 03:28Chama huru cha waandishi wa habari nchini Sudan kimetangaza kuwa, waandishi wa habari nchini humo wameamua kugoma ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono matakwa ya haki ya wananchi wanaopigania uhuru na demokrsia nchini humo. Hii ni katika hali ambayo serikali ya Abdel Fattah el Sisi ya Misri imetangaza kumuunga mkono Rais Omar al Bashir wa Sudan katika hali ngumu ya nchi hiyo hivi sasa.
-
'Maandamano ya Mkate' yazidi kuigubika Sudan, Rais al-Bashir akalia kuti kavu
Dec 27, 2018 11:28Maandamano ya mkate ambayo yamekuwa yakishushuhudiwa nchini Sudan kwa wiki moja sasa na ambayo yamechukua mkondo wa kisiasa, yamezidi kuigubika nchi hiyo na kuifanya serikali ya Rais Omar Hassan al-Bashir ikabiliwe na mashinikizo zaidi.
-
Rais al Bashir atishia kukata mikono ya waandamanaji Sudan
Dec 27, 2018 04:16Rais Hassan al Bashir wa Sudan amekemea vikali "maandamano ya mkate" yanayoendelea kwa zaidi ya wiki moja sasa nchini humo dhidi ya serikali yake na kusema kuwa atakata mikono ya waandamanaji hao.
-
Msudan mwingine auawa katika maandamano
Dec 26, 2018 09:52Baada ya kuuawa Msudan mwingine katika maandamano ya kupinga serikali, idadi ya wahanga waliopoteza maisha yao katika maandamano yaliyoanza wiki iliyopita, wameshafikia 38.
-
Amnesty: Watu 37 wameuawa katika 'maandamano ya mkate' Sudan
Dec 25, 2018 23:36Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema makumi ya watu wameuawa katika makabiliano baina ya polisi na waandamanaji nchini Sudan.
-
Jeshi la Sudan latangaza uungaji mkono kwa al Bashir, vyama vya upinzani vyajiunga na maandamano ya wananchi
Dec 24, 2018 23:29jeshi la Sudan limetangaza uungaji mkono wake kwa kiongozi anayezongwa na matatizo mengi ya kisiasa na kiuchumi wa nchi hiyo baada ya kushadidi maandamano ya wananchi wanaopinga hali mbaya ya uchumi. Waandamanaji hao pia wametoa wito wa kuondolewa madarakani serikali ya sasa ya Khartoum.