-
UN yasema machafuko mapya Sudan Kusini yanaongeza mateso kwa raia
Apr 30, 2017 03:01Umoja wa Mataifa umeeleza kusikitishwa na kuongezeka kwa machafuko na mateso kwa raia wa Sudan Kusini, kufuatia operesheni ya hivi karibuni ya jeshi la serikali ya nchi hiyo.
-
Baadhi ya marais wa Afrika hawataki Machar arejee Sudan Kusini
Apr 27, 2017 03:32Mjumbe wa Umoja wa Mataifa amesema baadhi ya nchi za kanda ya Afrika Mashariki pamoja na Afrika Kusini haziungi mkono wazo la kurejea mjini Juba, kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini, Riek Machar.
-
Sudan yamtuhumu Rais wa Sudan Kusini kwa kufanya mazungumzo na waasi
Apr 25, 2017 03:46Sudan jana iliitaka nchi jirani ya Sudan Kusini isitishe uungaji mkono wake kwa makundi ya waasi wanaopigana vita na Khartoum na kumtuhumu Rais Kiir kuwa amekutana na kufanya mazungumzo na waasi wiki iliyopita.
-
UN: Wafanyakazi 82 wa ufikishaji misaada wameuliwa katika vita vya ndani Sudan Kusini
Apr 20, 2017 02:34Mratibu mkaazi wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini amesema wafanyakazi 82 wa utoaji misaada wameuliwa katika vita vya ndani vya nchi hiyo na kwamba idadi ya raia waliobaki bila makaazi sasa imefikia milioni tatu na nusu.
-
Indhari ya Unicef kuhusu kusimamia utoaji huduma huko Somalia na Sudan Kusini
Apr 19, 2017 02:58Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetahadharisha kuhusu kukosekana usimamizi wa utoaji huduma za kibinadamu kwa raia wa Sudan Kusini na Somalia.
-
Wimbi la mauaji laendelea Sudan Kusini, 14 wauawa
Apr 16, 2017 02:44Kwa akali watu 14 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika mapigano mapya baina ya wanajeshi wa serikali na waasi katika mji wa Raga nchini Sudan Kusini.
-
WFP yalaani mauaji ya wafanyakazi wa ufikishaji misaada ya kibinadamu Sudan Kusini
Apr 14, 2017 22:00Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakuka Duniani (WFP) limelaani muaji ya wafanyakazi wake watatu wanaohudumu nchini Sudan Kusini.
-
Uingereza: Machafuko ya Sudan Kusini ni sawa na mauaji ya kimbari
Apr 14, 2017 03:48Waziri wa Serikali ya Uingereza amesema kuwa mauaji yaliyoyalenga makundi maalumu ya kikabila huko Sudan Kusini na kusababisha vita vya ndani nchini humo mwaka 2013, ni sawa na mauaji ya kimbari.
-
Watu 16 wauwa katika mapigano nchini Sudan Kusini
Apr 11, 2017 12:05Kwa akali watu 16 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika mapigano baina ya wanajeshi wa serikali na waasi nchini Sudan Kusini.
-
Wakimbizi wa Sudan Kusini: Askari 'wamewachinja raia kama wanyama'
Apr 08, 2017 11:22Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) limesema watu zaidi ya 6,000 wamekimbia makazi yao nchini Sudan Kusini na kukimbilia wilaya ya kaskazini mwa Uganda ya Lamwo kujisalimisha na mauaji ya raia yanayofanywa na askari wa serikali ya Juba.