Indhari ya Unicef kuhusu kusimamia utoaji huduma huko Somalia na Sudan Kusini
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i27974-indhari_ya_unicef_kuhusu_kusimamia_utoaji_huduma_huko_somalia_na_sudan_kusini
Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetahadharisha kuhusu kukosekana usimamizi wa utoaji huduma za kibinadamu kwa raia wa Sudan Kusini na Somalia.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Apr 19, 2017 02:58 UTC
  • Indhari ya Unicef kuhusu kusimamia utoaji huduma huko Somalia na Sudan Kusini

Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetahadharisha kuhusu kukosekana usimamizi wa utoaji huduma za kibinadamu kwa raia wa Sudan Kusini na Somalia.

Manuel Fontaine amesema kuwa watoto zaidi ya laki tano wanahitaji kupatiwa huduma za kibinadamu kikiwemo chakula huko Sudan Kusini na Somalia, hata hivyo amesema mapigano ya ndani na ukosefu wa amani vinakwamisha kushughulikiwa suala hilo. 

Afisa huyo anayehusika na Huduma za Dharura wa Unicef amebainisha kuwa serikali za Sudan Kusini, Somalia na Kikosi cha Kudumisha Amani cha Umoja wa Mataifa hazijatekeleza ahadi zao za kuwadhaminia usalama wafanyakazi wa huduma za kibinadamu.

Tangu kuanza mwaka huu wa 2017 hadi hivi sasa, jumla ya kesi 20 za watu wanaougua ugonjwa wa kipindupindu zimesajiliwa huko Somalia; kiwango ambacho kimetajwa kuwa ni cha asilimia 700 ikilinganishwa na mwaka jana katika kipindi kama hiki.

Wagonjwa wa kipindupindu wakipatiwa matibabu Sudan Kusini 

Ameongeza kuwa kesi nyingine za kipindupindu 5500 zilisajiliwa huko Sudan Kusini pia kuanzia mwezi Juni mwaka jana. Somalia imetumbukia katika hali ya mchafukoge na kuathiriwa na ukosefu wa amani kwa miongo mitatu sasa. Sudan Kusini ilijitenga na Sudan mwaka 2011 baada ya miongo kadhaa ya mapigano.