-
Mgogoro wa kisiasa Tunisia wazidi kutokota, Rais awatimua maafisa wengine wa serikali
Jul 29, 2021 06:35Tunisia imeendelea kutumbukia zaidi katika mgogoro mkubwa wa kisiasa baada ya Rais Kais Saied kuwafukuza kazi maafisa zaidi, siku chache tu baada ya kumtimua waziri mkuu, kusimamisha shughuli za Bunge na kuchukua madaraka yote ya kiutawala.
-
Saudi Arabia yaunga mkono mapinduzi baridi ya Rais wa Tunisia
Jul 28, 2021 22:02Saudi Arabia imeunga mkono uamuzi uliochukuliwa na Rais Kais Saied wa Tunisia wa kumfuta kazi aliyekuwa waziri mkuu na kuvunja Bunge la nchji hiyo ambao umetajwa kuwa ni mapinduzi baridi.
-
Chama cha Ennahdha chamtaka Rais wa Tunisia kutengua maamuzi yake
Jul 28, 2021 02:13Chama cha Ennahdha kimemtaka Rais wa Tunisia atengue maamuzi aliyochukua hivi karibuni ya kumfuta kazi waziri mkuu na kusitisha shughuli za Bunge la nchi hiyo.
-
Kutokea mapinduzi baridi nchini Tunisia
Jul 27, 2021 21:07Katika hatua inayotathminiwa na wajuzi wa mambo kama mapinduzi baridi, Rais Kais Saied wa Tunisia amechukua hatua kadhaa kama kumfuta kazi Waziri Mkuu wa nchi hiyo Hichem Mechichi, kuvunja baraza la mawaziri, kusitisha shughuli za Bunge na kinga ya kisiasa ya Wabunge na kisha kudhibiti madaraka yote ya nchi.
-
Iran: Tunafuatilia kwa karibu matukio yanayojiri Tunisia
Jul 27, 2021 20:59Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu inafuatilia kwa karibu matukio ya kisiasa yanayoendelea kushuhudiwa hivi sasa nchini Tunisia.
-
Polisi yaivamia ofisi ya Al Jazeera huko Tunis
Jul 26, 2021 22:49Mkuu wa ofisi ya televisheni ya al Jazeerahuko Tunis mji mkuu wa Tunisia amesema polisi wameivamia ofisi hiyo jana Jumatatu.
-
Rais wa Tunisia afanya mapinduzi baridi, amfuta kazi Waziri Mkuu, Spika wa Bunge
Jul 25, 2021 22:38Rais Kais Saied wa Tunisia amechukua hatua ya kushtukiza ya kumfuta kazi Spika wa Bunge na Waziri Mkuu wa nchi hiyo na kudhibiti madaraka yote ya nchi.
-
Wanaharakati wa nchi 5 za kaskazini mwa Afrika: Kuna udharura wa kukabiliana na mwenendo wa kuanzisha uhusiano na Israel
Jul 25, 2021 22:09Wanaharakati kutoka nchi tano za kaskazini mwa Afrika ambazo ni Algeria, Tunisia, Morocco, Libya na Mauritania wamesisitiza udharura wa kukabiliana na hatua ya baadhi ya nchi ya kuanzisha uhusiano rasmi wa na utawala ghasibu wa Israel.
-
Wahajiri 17 wapoteza maisha katika fukwe za Tunisia
Jul 22, 2021 03:26Shirika la Hilal Nyekundu la Tunisia limetangaza kuwa, wahajiri 17 wamekufa maji katika fukwe za nchi hiyo baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafiria kupinduka baharini.
-
Tunisia yakadhibisha kushiriki maneva ya Marekani na utawala wa Kizayuni katika Bahari Nyeusi
Jun 24, 2021 02:52Msemaji rasmi wa Wizara ya Ulinzi ya Tunisia amekadhibisha uvumi ulioenea katika vyombo vya habari kwamba nchi hiyo itashiriki katika maneva ya kijeshi na Marekani na utawala ghasibu wa Kizayuni katika Bahari Nyeusi.