Saudi Arabia yaunga mkono mapinduzi baridi ya Rais wa Tunisia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i72884-saudi_arabia_yaunga_mkono_mapinduzi_baridi_ya_rais_wa_tunisia
Saudi Arabia imeunga mkono uamuzi uliochukuliwa na Rais Kais Saied wa Tunisia wa kumfuta kazi aliyekuwa waziri mkuu na kuvunja Bunge la nchji hiyo ambao umetajwa kuwa ni mapinduzi baridi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 28, 2021 22:02 UTC
  • Saudi Arabia yaunga mkono mapinduzi baridi ya Rais wa Tunisia

Saudi Arabia imeunga mkono uamuzi uliochukuliwa na Rais Kais Saied wa Tunisia wa kumfuta kazi aliyekuwa waziri mkuu na kuvunja Bunge la nchji hiyo ambao umetajwa kuwa ni mapinduzi baridi.

Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Saudi Arabia imetangaza kuwa, Riyadh inaheshimu mambo yote yanayofungamana na masuala ya ndani ya Tunisia na inatambua kuwa yanahusu utawala na mamlaka ya nchi hiyo. Imeongeza  kuwa Saudia iko pamoja na inaunga mkono hatua yoyote ya kuimarisha utulivu katika nchi ya Tunisia.

Taarira ya hiyo ya Saudia imesema: "Riyadh inaamini kuwa uongozi wa Tunisia una uwezo wa kuvuka kipindi cha sasa na kutayarisha maisha bora na ya heshima kwa Watunisia; vilevile inaiomba jamii ya kimataifa kuisaidia Tunisia kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za kiafya na kiuchumi zinazoisumbua nchi hiyo kwa sasa." 

Tangu Jumapili iliyopita nchi ya Tunisia ilitumbukia katika mgogoro mkubwa wa kisiasa baada ya Rais Kais Saied wa nchi hiyo kumtimua Waziri Mkuu, Hichem Mechichi, kusitisha kazi za Bunge na kufuta kinga ya kisiasa na wabunge. 

Tunisia

Mapinduzi baridi ya Rais Kais Saied nchini Tunisia yamefanyika huku mamia ya watu wakifanya maandamano siku ya Jumapili kulalamikia hali mbaya ya kisiasa na ukosefu wa huduma za afya. 

Vilvile njia zote zinazoishia mji mkuu wa Tunisia, Tunis, zilifungwa, na idadi kubwa ya wanajeshi ilionekana katika barabara kuu za nchi hiyo.