-
Wananchi wa Tunisia waandamana tena dhidi ya Rais Kais Saied
Jan 15, 2023 06:55Kwa mara nyingine tena wananchi wa Tunisia wamefanya maandamano makubwa wakimtaka Rais Kais Saied wa nchi hiyo na serikali yake wajiuzulu, kwa kushindwa kuinasua nchi hiyo kutoka kwenye mgogoro wa kisiasa na hali mbaya ya kiuchumi na kijamii.
-
Mgomo mkubwa Tunisia; jibu la kutotekeleza ahadi Rais Kais Saied
Dec 30, 2022 02:33Muungano Sekta ya Usafiri na Uchukuzi wenye mfungamano na Muungano Mkubwa wa Wafanyakazi nchini Tunisia (UGTT) umetangaza mkakati wake wa kufanya mgomo wa siku mbili Januari 25 na 26 mwaka 2023.
-
Al-Ghannoushi: Uchaguzi wa Bunge la Tunisia ulikuwa jibu la "hapana" kwa Kais Saied
Dec 25, 2022 02:18Mkuu wa chama cha Kiislamu cha Ennahda nchini Tunisia amesema idadi ndogo ya waliojitokeza kupiga kura katika uchaguzi wa hivi karibuni wa Bunge ni ishara ya matakwa ya wananchi wanaomtaka rais huyo ajiuzulu.
-
Ushiriki mdogo wa wananchi wa Tunisia katika uchaguzi wa Bunge
Dec 19, 2022 12:47Karibu akthari ya watu waliotimiza masharti ya kupiga kura nchini Tunisia walisusia uchaguzi wa Bunge uliofanyika Jumamosi ya juzi tarehe 17 Disemba.
-
Upinzani wataka Rais wa Tunisia ajiuzulu kwa 'kususiwa' uchaguzi wa bunge
Dec 18, 2022 10:41Muungano mkubwa zaidi wa upinzani nchini Tunisia umemtaka Rais Kais Saied wa nchi hiyo ajiuzulu kutokana na ushiriki mdogo wa wananchi katika uchaguzi wa bunge uliofanyika jana.
-
Wananchi wa Tunisia wapiga kura katika uchaguzi wa bunge uliosusiwa na wapinzani
Dec 18, 2022 04:14Wananchi wa Tunisia jana Jumamosi walianza kupiga kura katika uchaguzi wa kwanza wa wabunge tangu Rais Kais Saied atangaze hatua za kipekee Julai 25 mwaka jana baada ya kulifuta kazi Bunge na kutwaa madaraka yote ya nchi. Vyama vya kisiasa na makundi ya upinzani yamesusia uchaguzi huo.
-
Hukumu ya Saudia Arabia dhidi ya daktari Mtunisia yapingwa na kulaaniwa vikali
Oct 24, 2022 07:37Taasisi ya Kitaifa ya Kuunga Mkono Muqawama na Kupinga Kuanzishwa Uhusiano wa Kawaida na utawala haramu wa Israel ya nchini Tunisia imelaani vikali hukumu ya Saudi Arabia ya kumfunga jela miaka 15 daktari mmoja wa kike raia wa Tunisia kwa kuweka video ya maandamano ya kuiunga mkono Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon.
-
Maelfu waandamana Tunisia kutaka rais Kais Saeid na serikali nzima wajiuzulu
Oct 16, 2022 02:30Wapinzani na wakosoaji wa rais Kais Saeid wa Tunisia wamefanya maandamano makubwa wakimtaka kiongozi huyo na serikali ya sasa ya nchi hiyo wajiuzulu.
-
Maiti 8 za wahajiri zapatikana pwani ya kusini ya Tunisia
Oct 11, 2022 11:51Wavuvi wa Tunisia wameopoa miili ya wahajiri wanane waliokufa maji katika pwani ya mji wa Zarzis, kusini mwa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
-
Tangazo la Rais wa Tunisia la marekebisho ya sheria ya uchaguzi
Oct 09, 2022 10:22Ofisi ya Rais wa Tunisia imetangaza katika taarifa yake kwamba Rais Kais Saied, ameamua kurekebisha sheria ya uchaguzi wa Bunge la nchi hiyo.