-
Raia wa Niger washambulia lori la Ufaransa lililokuwa limebeba maji
Sep 30, 2023 12:16Raia wa Niger wamelishambulia lori la Ufaransa lililokuwa limebeba maji kwa ajili ya wanajeshi wa nchi hiyo walioko nchini humo kinyume cha sheria.
-
Umoja wa Mataifa wakosoa hatua mpya ya Ufaransa dhidi ya hijabu ya Kiislamu
Sep 29, 2023 04:47Marta Hurtado, Msemaji wa Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, Jumatano alikosoa marufuku ya uvaaji hijabu kwa wanariadha wa Ufaransa katika michezo ya Olimpiki ya 2024, ambayo imepangwa kufanyika Paris mwaka ujao.
-
Umoja wa Mataifa wakosoa "marufuku ya hijabu" katika Michezo ya Olimpiki 2024
Sep 27, 2023 12:55Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imekosoa uamuzi wa serikali ya Ufaransa "kupiga marufuku vazi la hijabu kwa wanariadha wa Ufaransa" katika Michezo ya Olimpiki ya mwaka ujao inayoandaliwa na Paris.
-
Kusalimu amri Ufaransa mbele ya takwa la Niger
Sep 26, 2023 07:02Hatimaye, baada ya wiki kadha za vuta nikuvute, Ufaransa imesalimu amri mbele ya takwa la Niger na kutangaza kwamba, balozi wa Ufaransa nchini Niger, Sylvian Itte, atarejea Paris katika saa chache zijazo.
-
Ufaransa yakumbwa na maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi
Sep 25, 2023 01:29Maelfu ya wananchi wa Ufaransa jana Jumapili waliandamana katika mitaa mbalimbali ya mji mkuu Paris na katika miji mingine nchini humo wakilalamikia ubaguzi wa rangi wa kimfumo unaoendelea kushuhudiwa nchini humo.
-
Macron adai waliofanya mapinduzi Niger "wanamshikilia" balozi wa Ufaransa
Sep 16, 2023 04:40Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, alidai jana Ijumaa kwamba balozi wa nchi yake nchini Niger, Sylvain Itte, "anazuiliwa" na utawala wa kijeshi wa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika, akiashiria kwamba chakula anachokula ni "mgao wa chakula cha kijeshi."
-
Paris yaakiri kushindwa kwa sera zake za kikoloni barani Afrika
Sep 06, 2023 23:07Mapinduzi mtawalia yaliyotokea katika nchi kadhaa za Kiafrika kama Niger na Gabon, ambayo amepongezwa na kupokewa kwa shangwe na wananchi, yamegeuka kuwa harakati kubwa dhidi ya ukoloni mpya na mamboleo wa Ufaransa barani Afrika.
-
Makumi ya wanafunzi wa kike Waislamu Ufaransa warejeshwa majumbani kwa kuvaa abaya
Sep 05, 2023 23:44Katika siku ya kwanza ya mwaka wa masomo, skuli za umma nchini Ufaransa zimewarejesha majumbani wasichana kadhaa kwa kukataa kuvua mabaibui ya abaya yanayovaliwa na baadhi ya wanawake na wasichana wa Kiislamu. Hayo ni kwa mujibu wa Waziri wa Elimu wa nchi hiyo Gabriel Attal.
-
Maandamano ya kutaka kufukuzwa askari wa Ufaransa yashtadi Niger
Sep 02, 2023 07:39Maelfu ya wananchi wa Niger wamefanya maandamano katika mji mkuu Niamey, kuonyesha uungaji mkono wao kwa serikali ya kijeshi inayotawala hivi sasa, na kutaka kufukuzwa nchini humo wanajeshi na wanadiplomasia wa Ufaransa katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
-
Polisi wa Niger wanaendelea kuzingira ubalozi wa Ufaransa
Sep 01, 2023 23:14Polisi nchini Niger wanaendelea kuzingira majengo ya ubalozi wa Ufaransa mjini Niamey, huku Baraza la Kijeshi linalotawala nchi hiyo likichukua uamuzi wa kupiga marufuku shughuli za mashirika ya kimataifa na yasiyo ya kiserikali.