-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu: Uingereza ni chanzo cha vitisho Asia Magharibi
Dec 18, 2016 01:07Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu jana Jumamosi alihutubia kikao cha Maulidi ya Mtume Muhammad (saw) kilichohudhuriwa na viongozi wa Iran, wageni wanaoshiriki katika Mkutano wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu, mabalozi wa nchi za Kiislamu na watu wa matabaka mbalimbali na kusisitiza kuwa, katika siku chache zilizopita Waingereza na bila ya kuona aibu, waliitaja Iran kuwa ni tishio la eneo la Ghuba ya Uajemi ilhali nchi hiyo ndiyo chanzo cha vitisho, ufisadi na hatari za aina mbalimbali.
-
Mchanganuzi: US, UK na Israel zimezitelekeza Sudan mbili baada ya kuzitenganisha
Dec 15, 2016 10:43Katika hali ambayo Sudan Kusini inatimiza miaka mitatu ya mapigano, machafuko na uhasama, wachanganuzi wa mambo wanasema kuwa, Marekani, Uingereza na Israel zimeitelekeza nchi hiyo na jirani yake Sudan, licha ya kuhusika moja kwa moja katika mpango wa kuzitenganisha.
-
Silaha za Uingereza zinatumiwa na nchi watenda jinai za eneo
Dec 14, 2016 00:56Gazeti la The Guardian limeandika kuwa Uingereza ni muuzaji mkubwa wa pili wa silaha na zana za kijeshi duniani na mdhamini wa silaha nyingi zaidi zinazotumiwa katika vita vinavyoendelea katika eneo la Mashariki ya Kati.
-
Uingereza, Saudia zinaituhumu Iran kuficha nafasi yao haribifu ya kuunga mkono magaidi
Dec 12, 2016 01:23Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: "Matamshi dhidi ya Iran yaliyotolewa na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza na Saudia Arabia ni katika njama ya kujaribu kuficha nafasi yao haribifu ya uungaji mkono magaidi wakufurishaji."
-
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran yamwita balozi wa Uingereza ajieleze
Dec 10, 2016 13:51Balozi wa Uingereza mjini Tehran ameitwa katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwenda kujieleza kuhusu matamshi yaliyo dhidi ya Iran yaliyotolewa na Waziri Mkuu wa Uingereza mjini Manama, Bahrain.
-
Snowden: Marekani na Uingereza zilimfanyia ujasusi Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
Dec 09, 2016 04:19Nyaraka zilizotolewa na afisa wa zamani wa Wakala wa Usalama wa Taifa wa Marekani zimefichua kuwa mashirika ya kijasusi ya nchi hiyo na yale ya Uingereza yalizifanyia ujasusi nchi za Afrika ikiwa ni pamoja na Rais wa Kenya.
-
Al-Shehabi: Uingereza inataka kuimarisha uhusiano wake na madikteta wa eneo
Dec 08, 2016 12:33Katibu Mkuu wa Harakati ya Uhuru ya Bahrain amesema Uingereza inataka kuendeleza sera zake za kushupalia vita katika eneo la Mashariki ya Kati kwa ajili ya kujiongezea pato.
-
Wabahrain waandamana dhidi ya Waziri Mkuu wa Uingereza
Dec 08, 2016 04:43Wananchi wa Bahrain wamefanya maandamano kueleza ghadhabu zao dhidi ya Waziri Mkuu wa Uingereza ambaye yuko nchini humo kushiriki mkutano wa kila mwaka wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi (P)GCC.
-
Qassemi: Waziri Mkuu wa Uingereza anajipendekeza kwa nchi za Kiarabu
Dec 08, 2016 04:13Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amekosoa vikali matamshi ya chuki dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu, yaliyotolewa jana na Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May, katika mkutano wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi (P)GCC, na kusisitiza kuwa kauli hiyo inalenga kuzifurahisha na kuziridhisha nchi za Kiarabu za baraza hilo.
-
Uingereza, Marekani zinawatumia magaidi misaada ya silaha
Dec 06, 2016 00:08Marekani na Uingereza zinapanga mikakati mipya kuhusu namna ya kuwafikishia silaha magaidi katika maeneo wanayoyadhibiti ya Aleppo au Halab nchini Syria.