Waislamu wa Uingereza waandaa ratiba maalumu ya kuutangaza Uislamu
https://parstoday.ir/sw/news/world-i23149-waislamu_wa_uingereza_waandaa_ratiba_maalumu_ya_kuutangaza_uislamu
Waislamu wa Msikiti wa Lincoln wa eneo la East Midlands nchini Uingereza wameanzisha ratiba maalumu ya kuutangaza Uislamu kwa Waislamu na wasio Waislamu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 09, 2017 12:50 UTC
  • Msikiti wa Lincoln wa eneo la East Midlands nchini Uingereza.
    Msikiti wa Lincoln wa eneo la East Midlands nchini Uingereza.

Waislamu wa Msikiti wa Lincoln wa eneo la East Midlands nchini Uingereza wameanzisha ratiba maalumu ya kuutangaza Uislamu kwa Waislamu na wasio Waislamu.

Shirika la habari la RASA limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, Msikiti wa Lincoln kila mwaka una ratiba ya kuwakaribisha watu mbalimbali wasio Waislamu kwa ajili ya kuitangaza kwa njia za busara dini tukufu ya Kiislamu.

Ratiba hizo ambazo ni miongoni mwa shughuli za Jumuiya ya Waislamu ya Lincoln haiwahusu tu wasio Waislamu, bali hata Waislamu nao wanapata nafasi ya kuitambua zaidi dini yao kupitia ratiba hizo.

Mandhari nyingine ya Msikiti wa Lincoln ulioko katika mtaa wa Orchard, Midlands Mashariki nchini Uingereza

 

Dk. Tanweer Ahmed, mwenyekiti wa jumuiya hiyo amesema, fikra ya kufungua milango ya Msikiti wa Lincoln kwa ajili ya watu wa matabaka na dini mbalimbali inasaidia sana kuutangaza Uislamu na Waislamu.

Jumuiya ya Waislamu ya Lincoln tangu ilipoanzishwa nchini Uingereza hadi hivi sasa imekuwa ni kituo muhimu sana kwa ajili ya sherehe za kidini na shughuli mbalimbali za Kiislamu.