-
Rais wa Cuba: Mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni wa Israel Gaza ni fedheha kubwa
Dec 28, 2023 00:52Rais Miguel Diaz-Canel wa Cuba amelaani vikali mauaji ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza na kueleza kwamba, mauaji hayo ya kimbari ni kashfa na fedheha kwa ubinadamu.
-
WFP yasimamisha usambazaji wa chakula Sudan, mapigano yaenea
Dec 21, 2023 07:53Mpango wa Chakula Dunia (WFP) umesimamisha kwa muda utoaji na usambazaji wa chakula katika baadhi ya maeneo katika jimbo la al-Jazira katikati ya Sudan, huku mapigano yakipanuka na kuenea pande za mashariki na kusini mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum.
-
Umoja wa Mataifa wataka kuundwa Mahakama maalumu ya vita vya Gaza
Dec 20, 2023 04:21Huku mashambulizi na mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni wa Israel yakiendelea Gaza, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya kibinadamu ametoa wito wa kuundwa mahakama maalumu kuhusiana na vita hivyo.
-
Guterres: US iifutie Iran vikwazo ili JCPOA iendelee kutekelezwa
Dec 19, 2023 23:35Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameitaka Marekani iiondolee vikwazo sekta ya mafuta ya Iran ili makubaliano ya nyuklia ya JCPOA ambayo Washington ilijiondoa kwayo Mei mwaka 2019 yaendelee kutekelezwa.
-
Barua isiyo ya kawaida ya Guterres kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Gaza
Dec 07, 2023 08:28Katika hatua isiyo ya kawaida, Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametumia mamlaka aliyopewa kisheria kupitia kifungu cha 99 cha Hati ya Umoja wa Mataifa kulishinikiza Baraza la Usalama la umoja huo lianzishe haraka usitishaji vita huko katika Ukanda wa Gaza.
-
Guterres atumia Ibara nadra ya UN kutuma ujumbe mzito kwa Baraza la Usalama kuhusu Gaza
Dec 07, 2023 03:36Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametumia ibara ya 99 ya Hati ya Umoja wa Mataifa, ambayo ni nadra sana kutumiwa na Katibu Mkuu wa umoja huo, kulitolea wito mzito Baraza la Usalama wa "kushinikiza kuepusha janga la kibinadamu" katika Ukanda wa Gaza na kuungana katika kutoa wito wa kusitishwa kikamilifu mapigano kati ya utawala wa Kizayuni wa Israel na Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS.
-
Visa vya utesaji watu Burundi vyaitia hofu UN, yataka hatua zichukuliwe
Nov 25, 2023 22:54Kamati ya Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu dhidi ya Utesaji, CAT imetamatisha kikao chake cha 78 mjini Geneva, Uswisi kwa kutoa mahitimisho ya ripoti za mataifa sita ikiwemo Burundi ambayo inaonesha wasiwasi juu ya utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa dhidi ya Mateso na adhabu za kikatili zisizoheshimu utu.
-
UN hatimaye yakubali kuondoa askari wake DRC baada ya miongo 2
Nov 22, 2023 23:36Umoja wa Mataifa umesaini makubaliano na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuhusu kuondoka kwa ujumbe wa umoja huo wa kulinda amani nchini humo (MONUSCO).
-
UN yataka Israel iruhusu wakaguzi huru kuingia Al Shifa
Nov 18, 2023 08:41Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ameitaka Israel iruhusu wakaguzi wake kuingia katika Hospitali ya Al-Shifa ili kuchunguza madai ya utawala wa Kizayuni eti ya kuwepo makao makuu ya HAMAS ndani ya hospitali hiyo.
-
Azimio la Baraza la Usalama kuhusu vita vya Gaza: Makubaliano ya kiwango cha chini
Nov 16, 2023 23:47Uzembe wa Umoja wa Mataifa na hasa mkwamo katika Baraza la Usalama la umoja huo ambao una jukumu muhimu la kulinda amani na usalama wa kimataifa, kuhusu vita vya Gaza, jinai za kivita na mauaji ya kimbari ya Wapalestina yanayofanywa na utawala wa Kizayuni, umekosolewa vikali kimataifa.