UN yataka Israel iruhusu wakaguzi huru kuingia Al Shifa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i104930-un_yataka_israel_iruhusu_wakaguzi_huru_kuingia_al_shifa
Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ameitaka Israel iruhusu wakaguzi wake kuingia katika Hospitali ya Al-Shifa ili kuchunguza madai ya utawala wa Kizayuni eti ya kuwepo makao makuu ya HAMAS ndani ya hospitali hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 18, 2023 08:41 UTC
  • UN yataka Israel iruhusu wakaguzi huru kuingia Al Shifa

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ameitaka Israel iruhusu wakaguzi wake kuingia katika Hospitali ya Al-Shifa ili kuchunguza madai ya utawala wa Kizayuni eti ya kuwepo makao makuu ya HAMAS ndani ya hospitali hiyo.

Volker Türk, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema: Utawala wa Kizayuni wa Israel lazima uipe nafasi timu ya shirika hilo kuchunguza madai kwamba HAMAS ilikuwa ikitumia Hospitali ya Al-Shifa kama 'kamandi ya kivita'. Israel ilidai kuwa kamandi ya vita ya HAMAS  iko eneo la chini ya hospitali hiyo kubwa zaidi ya Ukanda wa Gaza, ambayo imekuwa ikishambuliwa mara kwa mara na jeshi la Israel.

Akijibu swali kuhusu madai na shutuma za jeshi la Israel kwamba HAMAS imeigeuza Hospitali ya Al-Shifa kuwa makao makuu ya kamandi ya jeshi na mahali pa kuficha silaha, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema: Tunahitaji kuingia ndani ya Hospitali ya Al Shifa.

Volker Türk amesisitiza kuwa: Hali kama hii inahitaji uchunguzi huru wa kimataifa kwa sababu tuna riwaya tofauti.

Volker Türk

Volker pia amesema: Hospitali ziko chini ya ulinzi maalumu wa sheria na sheria za kimataifa katika hali yoyote ile.

Mashambulizi dhidi ya hospitali ni kinyume cha sheria za kimataifa na Mikataba ya Geneva inayotaja vituo vya matibabu kama miundombinu ya kiraia.

Harakati ya HAMAS imeutaka Umoja wa Mataifa kuunda timu ya uchunguzi ili kufichua madai ya Tel Aviv kuhusu hospitali hiyo.

Waziri Mkuu wa Israel amelazimika kujitoa kimasomaso baada kukumbwa na mashinikizo makubwa kufuatia amri yake ya kuvamiwa Hospitali ya Al Shifaa na wanajeshi makatili wa Israel.

Awali Wazayuni walidai kuwa HAMAS imezigeuza hospitali za Ghaza kuwa kambi zake za kijeshi, na baada ya kukosa ushahidi wa kuhalalisha jinai na mashambulizi yake kwenye hospitali hizo, wamedai kuwa, HAMAS ilikuwa imeficha mateka wa Kizayuni kwenye hospitali hizo, na hivi sasa baada ya kuthibitika uongo wao, Benjamin Netanyahu anadai kuwa eti walikuwa na taarifa za uhakika kuwa mateka wamefichwa hospitalini.