-
Kwa mara ya kwanza, Mahakama ya Uhispania yachunguza jinai za Netanyahu na wenzake
Jul 08, 2025 16:04Mahakama ya Taifa ya Uhispania imeanzisha uchunguzi wa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu anaoshutumiwa kuufanya waziri mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu, waziri wake wa vita Israel Katz, na maafisa kadhaa waandamizi wa jeshi la utawala huo haramu hususan shambulio la mwezi uliopita lililofanywa jeshi la kizayuni dhidi ya meli ya misaada ya kibinadamu.
-
Trump na Netanyahu wajadili kuwahamisha Wapalestina kwa nguvu Ghaza
Jul 08, 2025 15:59Waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu amekutana na Rais wa Marekani Donald Trump katika Ikulu ya White House, huku viongozi hao wawili wakirudia pendekezo lao tata la kuwahamisha kwa nguvu maelfu ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza.
-
Israel yaharakisha kuifanya kaskazini ya Ghaza ibaki bila wakazi kabla vita kusimamishwa
Jul 06, 2025 19:34Duru za kuaminika za Palestina zimeripoti kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unaharakisha kuhawamisha wakazi wa kaskazini ya Ghaza ili eneo hilo libaki tupu kabla ya kusimamishwa vita endapo mwafaka utafikiwa.
-
Watu wa Uholanzi waandamana kupinga kutumwa vipuri vya ndege za kivita za F-35 kwa Israel
Jul 06, 2025 07:52Wananchi wa Uholanzi wamefanya maandamano wakipinga hatua ya kampuni ya Uholanzi ya kutuma vipuri vya ndege za kivita za F-35 kwa utawala wa Israel.
-
Wanahabari mashuhuri walaani upendeleo wa BBC unaoiunga mkono Israel
Jul 04, 2025 03:22Kundi la wafanyakazi wa BBC na mamia ya wanahabari na watu mashuhuri wameandika barua ya wazi kwa wasimamizi wa shirika la BBC, wakikosoa upendeleo wa wazi wa tasisi hiyo katika kuakisi matukio ya vita vya Gaza na kuonya kwamba BBC imekuwa msemaji wa propaganda za utawala wa Israel.
-
UN: Israel imekiuka sheria za kimataifa kwa kuwalenga raia wa Iran
Jul 02, 2025 02:44Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa imetangaza kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel umekiuka pakubwa sheria za kimataifa kwa kuwaua shahidi wanafamilia wa wanasayansi wa nyuklia na raia wa kawaida wa Iran.
-
Papa Leo aikemea Israel kwa kutumia njaa kama wenzo wa vita
Jul 01, 2025 12:31Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani kwa mara kadhaa sasa tangu achaguliwe kuongoza kanisa Katoliki ameutahadharisha utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu kutumia njaa kama wenzo wa kivita katika Ukanda wa Gaza.
-
Hamas: Muqawama utaendelea kukabiliana na mashambulizi ya Israel
Jul 01, 2025 12:25Afisa wa ngazi ya juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) ameonya kuwa kuendelea mashambulizi na hujuma za Israel kunazidisha mapambano na muqawama wa wananchi wa Palestina dhidi ya maghasibu Wazayuni.
-
Mashambulio ya makombora na ndege zisizo na rubani ya Iran dhidi ya Israel, mwisho wa zama za "kushambulia na kukimbia" kwa Israel.
Jun 15, 2025 12:15Baada ya utawala wa Kizayuni kuishambulia Iran kwa ushirikiano wa Washington asubuhi ya Ijumaa, Juni 13, na kupelekea kuuawa shahidi idadi kubwa ya makamanda waandamizi wa kijeshi na wanasayansi, pamoja na raia wa kawaida, Iran, kama ilivyoahidi awali, ilianza kutoa jibu kali kwa jinai hiyo na mauaji ya kimbari Ijumaa usiku kupitia operesheni ya mashambulio ya makombora na ndege zisizo na rubani, iliyopewa jina la Ali ibn Abi Talib.
-
Kwa nini Marekani imewawekea vikwazo majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai?
Jun 08, 2025 06:45Marekani mnamo Alhamisi, Juni 5, iliwawekea vikwazo majaji wanne wa kike wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai kwa kushughulikia kesi zinazohusiana na Israel na hatua za Marekani nchini Afghanistan. Vikwazo hivyo, ambavyo mara nyingi huwekewa maafisa kutoka nchi zinazopinga Marekani, sasa vimewalenga maafisa wa mahakama ya kimataifa.