-
Balozi wa utawala wa Kizayuni atimuliwa Colombia
Jun 24, 2024 03:34Balozi wa Israel ametimuliwa nchini Colombia baada ya Bogota kuvunja uhusiano wake wa kidiplomasia na utawala wa Kizayuni kutokana na mashambulizi na jinai zisizokwisha za Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina hasa wa Ukanda wa Ghaza.
-
Jibu la Hizbullah litaurejesha utawala wa Israel katika Zama za Mawe
Jun 23, 2024 04:07Kituo cha Taarifa za Vita cha Hizbullah ya Lebanon kimetangaza kuwa, shambulio kali la harakati hiyo ya muqawama dhidi ya vituo nyeti vya utawala wa Kizayuni, ambavyo vinajulikana tu na vyombo vya usalama vya utawala huo, litairejesha Israel katika zama za mawe.
-
Umoja wa Mataifa watoa onyo kali kuhusu kuongezeka majanga katika Ukanda wa Gaza
Jun 20, 2024 22:44Francesca Albanese, Ripota wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Palestina, amesema katika taarifa kwamba hali ya maafa huko Ukanda wa Gaza imezidi kuwa mbaya. Kwa kauli yake, utawala haramu wa Israel unalenga misafara ya misaada ya kibinadamu inayotumwa Gaza na kuzuia ufikaji wa misaada katika ukanda huo.
-
HAMAS yaitaka jamii ya kimataifa kuwasaidia watu wa Gaza
Jun 18, 2024 23:51Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetoa mwito wa kupitishwa maamuzi ya dharura na jamii ya kimataifa ya kusimamisha jinai za utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza na kuwasaidia wananchi wa ukanda huo wanaokabiliwa na masaibu mengi.
-
Iran yaonya kuhusu chokochoko yoyote tarajiwa ya Israel katika mipaka ya Lebanon
Jun 14, 2024 04:03Kaimu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameuonya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya chokochoko yake yoyote tarajiwa katika mipaka ya Lebanon.
-
Yaliyoifanya Marekani ipendekeze katika Baraza la Usalama la UN azimio la kusitishwa vita Ghaza
Jun 12, 2024 22:40Marekani ambayo huko nyuma ilionyesha waziwazi kuwa ndiye muungaji mkono mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kuyapigia kura ya turufu mara kadhaa maazimio tofauti ya Umoja wa Mataifa ya kusitisha vita katika Ukanda wa Ghaza, hatimaye siku ya Jumatatu Juni 10 iliwasilisha azimio jipya la usitishaji vita ambalo lilipitishwa na Baraza la Usalama kwa kura 14 kati ya 15 zilizounga mkono, ukiondoa Russia tu iliyoamua kutopiga kura.
-
HAMAS yatoa pigo jingine angamizi dhidi ya wanajeshi wa Israel
Jun 11, 2024 03:55Brigedi za Shahid Izzuddin al Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS zimetoa pigo jingine kubwa kwa wanajeshi vamizi wa Israel katika mji wa Rafah wa kusini mwa Ukanda wa Ghaza.
-
Mufti wa Oman awataka Waislamu kujitokeza kwa wingi kuwasaidia ndugu zao wa Ghaza
Jun 10, 2024 07:38Mufti Mkuu wa Oman, Sheikh Ahmed bin Hamad Al-Khalili amewataka Waislamu kote ulimwenguni kutumia sehemu ya fedha zao kuwapelekea msaada wa chakula na silaha Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza
-
HAMAS: Mateka watatu, akiwemo raia wa US, waliuawa katika shambulio la Israel Nuseirat
Jun 10, 2024 04:36Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema mateka watatu waliuawa akiwemo raia wa Marekani katika shambulio la kinyama lililofanywa hivi karibuni na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel kwenye kambi ya wakimbizi wa Kipalestina ya Nuseirat huko Ghaza, lililoua pia zaidi ya raia 270 wa Kipalestina.
-
Gantz ajiuzulu na kujitoa kwenye baraza la mawaziri la vita la utawala wa Kizayuni
Jun 10, 2024 03:20Benny Gantz, mjumbe wa baraza la mawaziri la vita la Israel, ametangaza rasmi kujiuzulu na kujitoa kwenye baraza hilo na kutoa wito wa kuitishwa uchaguzi wa mapema.