Jun 14, 2024 07:33 UTC
  • Iran yaonya kuhusu chokochoko yoyote tarajiwa ya Israel katika mipaka ya Lebanon

Kaimu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameuonya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya chokochoko yake yoyote tarajiwa katika mipaka ya Lebanon.

Ali Bagheri Kani, amesema hayo katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Iraq, Qassem al-A'raji ambapo ameeleza kuwa, Wazayuni hawana kumbukumbu nzuri kuhusu Lebanon na kwamba mchakato wa kushindwa utawala ulishaanza kutokea Lebanon, na kuongeza kuwa Lebanon itakuwa Jahanamu isiyo na marejeo kwa Wazayuni.

Kaimu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran aidha amesema kuwa, Wazayuni kwa kufanya mauaji dhidi ya Wapalestina wanataka kurejea katika hali yao ya kabla ya tarehe 7 Oktoba 2023, lakini hali ya mambo haitarejea kama ilivyokuwa kabla ya hapo.

Ali Bagheri Kani Kaimu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran akiwa katika mazungumzo na Rais Abdul Latif Rashid wa Iraq

 

Utawala wa Kizayuni wa Israel umeendeleza mashambulizi yake ya kikatili dhidi ya Gaza licha ya azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutaka kusitishwa mapigano mara moja katika eneo hilo la Palestina lililowekeza mzingiro.

Miezi minane ikiwa imepita tangu utawala wa Kizayuni ulipoanzisha vita vya kikatili dhidi ya Gaza, sehemu kubwa ya majengo ya eneo hilo yamegeuka magofu huku jeshi la Kizayuni likiendelea kuweka kizuizi cha kufikishwa chakula, maji safi na dawa kwa wakazi wa eneo hilo wanaoatilika kwa njaa.

Tags