-
Mamia ya watu wanaandamana Afrika Kusini kupinga chuki dhidi ya wageni
Aug 09, 2026 11:04Mamia ya watu wameandmana katika miji mbalimbali nchini Afrika Kusini wakitaka kukomeshwa ghasia dhidi ya wahamiaji, ambazo zimewalazimisha makumi ya maelfu ya watu kukimbia nchi hiyo.
-
Algeria na Italia zakubaliana kuimarisha ushirikiano ili kupambana na uhamiaji haramu
Aug 04, 2026 10:19Algeria na Italia zimekubaliana kuimarisha ushirikiano dhidi ya uhamiaji haramu na uhalifu wa kuvuka mipaka. Uamuzi huu umefikiwa wakati wa mazungumzo kati ya Mawaziri wa Mambo ya Ndani wan chi mbili hizo huko Roma, Italia.
-
Watu kadhaa wafa maji, mamia ya Wamorocco wakimbilia Ceuta ya Uhispania
Jul 31, 2026 08:37Wimbi la wahamiaji kutoka Morocco kuelekea mji unaodhibitiwa na Uhispania wa Ceuta limegeuka kuwa mgogoro wa kibinadamu na kisiasa, baada ya miili ya wahamiaji tisa kuopolewa majini. Wahamiaji hao waliaga dunia wakiwa katika jitihada za kuogelea hadi mjini huo.
-
Waghana waiomba ICC kuchunguza ukatili wa chuki dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini
Jul 24, 2026 02:48Raia wawili wa Ghana wamewasilisha ombi kwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) wakiitaka kufungua uchunguzi wa awali kuhusu vitendo vya ukatili vinavyowalenga wageni nchini Afrika Kusini, wakisema kwamba muundo, ukubwa na kukaririwa mashambulizi yanayowalenga wahamiaji vinaweza kuwa uhalifu dhidi ya ubinadamu.
-
Raia wa Zimbabwe warejea nyumbani kutoka Afrika Kusini huku ghasia dhidi ya wahamiaji zikiendelea
Jul 13, 2026 03:03Raia wa Zimbabwe wanaokimbia vurugu na vitisho vya chuki dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini wamewasili katika kituo cha mapokezi katika mji wa mpakani wa Beitbridge, Zimbabwe.
-
Nigeria na Afrika Kusini zavutana kwa kifo cha raia katika seli za polisi
Jul 09, 2026 11:36Polisi ya Afrika Kusini imethibitisha kuwa kifo cha raia wa Nigeria akiwa korokoroni hakikutokana na maandamano dhidi ya wahamiaji wa kigeni nchini humo yaliyofanyika wiki iliyopita.
-
Ghasia dhidi ya wahamiaji Afrika Kusini zatarajiwa leo
Jun 30, 2026 03:42Afrika Kusini inakabiliwa na mtihani mkubwa wa kiusalama baada ya magenge ya wahalifu kuapa kuwatimu raia wa kigeni nchini humo kuanzia leo.
-
Afrika Kusini yaapa kukabiliana vikali na ukatili dhidi ya wahamiaji
Jun 26, 2026 11:10Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, ameapa kukabiliana na jaribio lolote la kuyumbisha taifa wakati wa maandamano yaliyopangwa kufanywa wiki ijayo dhidi ya wahamiaji, huku wimbi la chuki dhidi ya wageni lizidi kuongezeka nchini humo.
-
Serikali ya Afrika Kusini yasema imewarejesha nyumbani wageni 2,745 ndani ya wiki moja
Jun 15, 2026 12:20Afrika Kusini imewarejesha nyumbani wageni 2,745 katika wiki moja baada ya Rais Cyril Ramaphosa kuapa kuchukua hatua kali dhidi ya uhamiaji haramu.
-
Kundi la kwanza la Waghana lawasili Accra baada ya kurejeshwa kutoka Afrika Kusini
May 28, 2026 11:55Kundi la kwanza la karibu Waghana 300 waliorudishwa kutoka Afrika Kusini kutokana na hujuma za kupinga wahamiaji, liliwasili Accra jana Jumatano.