-
Wabunge wa Iran wakusanya sahihi kumsihi Zarif asijiuzulu
Feb 27, 2019 08:00Wabunge wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) wameanza kukusanya sahihi kwa shabaha ya kumuomba Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran aghairi msimamo wake wa kujiuzulu.
-
Iran yakosoa undumakuwili wa nchi za Magharibi kuhusu haki za binadamu
Feb 18, 2019 02:33Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekosoa sera za nchi za Magharibi za uuzaji silaha na vigezo vya haki za binadamu vilivyojaa undumakuwili.
-
Zarif: Vikwazo haviwezi kutenganisha wananchi wa Iran na serikali yao
Feb 13, 2019 07:39Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema mashinikizo na vikwazo vya Marekani na nchi za Magharibi kwa ujumla vimeshindwa kulipigisha magoti taifa la Iran na kwamba katu njama hizo haziwezi kuwatenganisha Wairani na serikali yao.
-
Zarif: Iran haitazisubiri nchi za Ulaya katika mabadilishano ya kifedha
Feb 05, 2019 04:46Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amesema katika suala la mabadilishano ya kifedha, Iran haitazisubiri nchi za Ulaya. Aidha amesisitiza kuwa, mfumo uliozinduliwa wa kuunga mkono mabadilishano ya kibiashara kati ya Iran na Ulaya ni wa majaribio na inasubiriwa kuona ni vipi nchi za Ulaya zinalipa uzito suala hilo.
-
Kumalizika safari ya Zarif nchini Iraq; dhihirisho la urafiki kuanzia Baghad hadi Arbil
Jan 18, 2019 11:13Safari ya siku tano ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Baghdad na kukutana kwake na viongozi wa serikali kuu mjini Baghdad na wa eneo la Kurdistan nchini humo ni ishara inayodhihirisha wazi kwamba uhusiano wa nchi mbili hizi jirani ni wa kirafiki.
-
Zarif: Kongamano lijalo la Marekani dhidi ya Iran huko Poland ni sarakasi
Jan 12, 2019 07:43Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu amesema mkutano wa Marekani na waitifaki wake dhidi ya Iran unaotazamiwa kufanyika mwezi ujao katika mji mkuu wa Poland, Warsaw ni mwendelezo wa michezo ya kuigiza na sarakasi za Wasington.
-
Marekani; sababu kuu ya ukosefu wa amani katika Mashariki ya Kati
Jan 11, 2019 01:13Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kadiri Wamarekani watakavyoondoka haraka nchini Syria ndivyo itakavyokuwa bora kwa wananchi wa nchi hiyo.
-
Zarif: Kilichosalia ni utawala wa Trump na utawala wa Israeli kujiondoa katika sayari ya dunia
Jan 02, 2019 07:15Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Mohammad Javad Zarif ameashiria uamuzi wa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel kujiondoa rasmi katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNSECO) na kusema kitu pekee kilichobakia sasa ni kujiondoa kwao katika sayari ya dunia.
-
Zarif: Iran katu haitafanya mazungumzo kuhusu makombora yake
Dec 15, 2018 14:43Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amesisitiza kwa mara nyingine kuwa, Iran haitafanya mazungumzo kuhusu makombora yake ya kujihami.
-
Marekani na waitifaki wake; wabebaji dhima na masuulia ya matatizo ya Mashariki ya Kati
Dec 14, 2018 16:47Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: Si Iran, bali ni Marekani na waitifaki wake ndio wahusika na wabeba dhima ya masaibu na matatizo yaliyolikumba eneo la Mashariki ya Kati, kuanzia yale yaliyosababishwa na Saddam mpaka yaliyoletwa na kundi la kigaidi la DAESH (ISIS).