-
Marekani: Vikwazo dhidi ya Zimbabwe vitaendelea kuwepo
Sep 14, 2018 15:45Serikali ya Marekani haitaondoa vikwazo ilivyoiwekea Zimbabwe hadi pale serikali mpya ya Rais Emmerson Mnangagwa wa nchi hiyo itakapodhihirisha kuwa inabadili mielekeo yake. Hayo yameelezwa na afisa wa ngazi ya juu wa masuala ya uchumi wa Marekani.
-
Polisi ya Zimbabwe yapiga marufuku mikusanyiko mjini Harare baada ya kuenea kipindupindu
Sep 13, 2018 07:41Polisi ya Zimbabwe imepiga marufuku mikusanyiko ya aina yoyote ile katika mji mkuuu Harare baada ya kipindipindu kusambaa mjini humo na kuua watu wasiopungua 21 hadi sasa.
-
Zimbabwe yatangaza hali ya hatari baada ya kuzuka kipindupindu katika mji mkuu Harare
Sep 12, 2018 03:53Serikali ya Zimbabwe imetangaza hali ya hatari baada ya kuibuka maradhi ya kipindupindu katika mji mkuuu Harare.
-
Waba waua watu 18 nchini Zimbabwe
Sep 11, 2018 10:11Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Afya wa mji mkuu wa Zimbabwe, Harare ametangaza kuwa mlipuko wa magonjwa ya kipindupindu na homa ya matumbo umeua watu wasiopungua 18 katika jiji hilo katika wiki moja iliyopita.
-
Kipindupindu chaua watu 16 katika mji mkuu wa Zimababwe, Harare
Sep 11, 2018 07:13Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Huduma za Afya na Tiba katika mji mkuu wa Zimbabwe, Harare amesema watu wasiopungua 16 wamefariki dunia wiki iliyopita kutokana na mripuko wa ugonjwa wa kipindupindu.
-
UN: Msaada wa haraka unahitajika kwa waathirika wa baa la njaa Zimbabwe
Sep 03, 2018 14:11Msemaji wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) amesema kuwa shirika hilo linahitajia msaada wa haraka wa zaidi ya tani milioni moja za chakula kwa ajili ya raia walioathiriwa na baa la njaa nchini Zimbabwe.
-
Mahakama Zimbabwe yatupilia mbali madai ya wapinzani, yaidhinisha ushindi wa Mnangagwa kama rais
Aug 24, 2018 14:42Mahakama ya Katiba nchini Zimbabwe imetupilia mbali kesi iliyokuwa imefunguliwa na wapinzani na kumuidhinisha Emmerson Mnangagwa kama rais wa nchi hiyo. Chama kikuu cha upinzani cha MDC kilikuwa kimepinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika mwezi uliopita wa Julai kwa madai ya kuwepo wizi wa kura.
-
Mbivu mbichi kujulikana leo Zimbabwe kuhusu ushindi wa Rais Emmerson Mnangagwa
Aug 24, 2018 08:20Raia wa Zimbabwe wana shauku kubwa ya kujua hukumu inayotazamiwa kutolewa na Mahakama ya Katiba ya nchi hiyo kuhusu kesi iliyowasilisha na kiongozi wa upinzani, Nelson Chamisa kupinga ushindi wa Rais Emmersom Mnangagwa katika uchaguzi uliofanyika Julai 30 mwaka huu.
-
Mbunge wa Uganda Bobi Wine kufikishwa katika mahakama ya kijeshi leo
Aug 23, 2018 04:47Mbunge wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi kwa jina maarufu Bobi Wine leo anatarajiwa kurudishwa katika mahakama ya kijeshi mjini Gulu kaskazini mwa nchi hiyo.
-
Mahakama ya Katiba Zimbabwe yaanza kusikiliza kesi kuhusu uchaguzi wa rais
Aug 22, 2018 07:53Mahakama ya Katiba nchini Zimbabwe inaanza kusikiliza leo, kesi ya chama kikuu cha upinzani MDC kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi rais Emmerson Mnangangwa.